ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, March 29, 2020

SHANGA NA BALAA LA CORONA IN NEW ORLEANS.

BY MOHAMED MATOPE

Shanga kwa waswahili ni ishara ya ya urembo na mahaba. Lakini pia shanga zinatumika sehemu nyingi duniani kwa namna tofauti. Kwa mfano in New Orleans, shanga zinatumika kwenye sherehe za Mardi Gras.

Labda ngoja nianze na history ya New Orleans. New Orleans ni mji mkubwa katika state ya Louisiana. State ya Louisiana ilikuwa ni territory ya Ufaransa mpaka mwaka 1803 baada ya Napoleon Bonaparte, raisi wa Ufaransa, kuiuza kwa USA kwa $15 million.

Kama nchi nyingi za afrika zilivyokuwa influenced na mkoloni kiutamaduni na lugha , Luisiana , imekuwa influence na French culture. Mitaa ya Louisiana na nyumba zao zimefanana na za ufaransa. Na kama wafaransa walivyo na tabia ya kula raha na fashion, watu wa Luisiana pia wanapenda tumbua maisha na kuvaa vizuri. Hii imesababisha mji wa New Orleans uwe na fine restaurants, clubs na bars kama Paris .

Sherehe ya Mardi Gras inafanyika kila mwaka in New Orleans toka mwaka 1837. Mardi Gras ni carnival, inayokusanyisha watu toka pembe zote ulimwenguni kuonyesha culture zao kwenye mitaa ya New Orleans. Mardi Gras vilevile inaeleweka kama the greatest free show on earth. Watu karibu 2 million huwa wanafurika New Orleans kuja sherehekea. Vijana wengi toka nchi mbalimbali huwa wanamiminika New Orleans kuja kutumbua maisha, ku party na kutafuta wachumba. Mardi Gras vilevile inaitwa beads and throw . Shanga ni sehemu kubwa ya hii sherehe.

Mardi Gras ya mwaka huu zilipangwa ifanyike February,25.
Wakati wa maandalizi ya sherehe , Meya wa New Orleans na city council walikaa chini na kuamua kama waairishe sherehe kwa ajili ya corona outbreak. Kumbuka hizi sherehe zinaleta sehemu kubwa ya uchumi wa New Orleans, kama ilivyo korosho ilivyo kwenye mkoa wa Mtwara. Kutupa shimoni zaidi ya $3 bilioni ilikuwa ni headache kwa viongozi wa jiji la New Orleans. Meya na watu wake wakaamua kufuata corona guidelines za federal government ambazo zilikuwa nyepesi. At that time kulikuwa na chini ya wagonjwa 50 wa corona nchini na vifo 15. Vile vile Trump alisema number of corona cases will go down quickly. Kitu ambacho Meya na watu wake hawakujua ni kuwa, walikuwa wanaamua jambo ambalo watalijutia maishani mwao.

Sherehe za Mardi-Gras zikafanyika kama zilivyopangwa. Kwenye hii sherehe watu huwa wanatembea mitaani na costume za nchi tofauti huku wakirusha shanga . Shanga zaidi ya million 10 zilirushwa na kuvaliwa mwaka huu . Kitu ambacho raia wa New Orleans walikuwa hawajui ni kuwa walikuwa hawadaki shanga peke yake , bali walikuwa pia wanadaka na kuvaa coronavirus. Mkusanyiko wa watu million 2 kutoka sehemu tofauti nchini na duniani, kupiga millions of selfies, na kusongamana kwenye mabaa na migahawa ni mazingira tosheleza kwa kueneza maambukizo ya coronavirus.

Hatima yake coronavirus ikaanza sambaa New Orleans kama mchwa. In March 9, exactly 2 weeks baada ya Mardi Gras, New Orleans ikapata case ya kwanza ya corona. Baada ya wiki mbili ikawa na case 576 za corona. Takwimu za leo , mwezi mmoja baada ya Mardi Gras zinaosnyesha New Orleans inawagonjwa 3,300+ na vifo 150+. Na New Orleans umekuwa mji wenye fastest growth za coronavirus cases in USA. Na pia, umekuwa ni mji unaoshikilia rekodi ya kuwa na wagonjwa wengi wa corona per capital duniani. Vilevile upo njiani kuwa the next national corona epicenter. Shanga zimeleta mambo.

Nimeandika hii article kwa kutumia vichekesho lakini point yangu ni kuwaelimisha watu jinsi coronavirus inavyoenea kiurahisi. Na pia kuwakumbusha viongozi wetu kuwa decision zao wanazochukuwa kupambana na hili gonjwa zina impact kubwa kwenye afya na maisha ya wananchi.

No comments: