ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, March 25, 2020

Sherehe, vijiwe vya kunywa mbege marufuku wilayani Rombo kwa sababu ya corona

By Janeth Joseph, Mwananchi jjoseph@mwananchi.co.tz

Rombo. Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Agness Hokororo amepiga marufuku mikusanyiko ya watu katika maeneo inakouzwa pombe aina ya mbege, sherehe za harusi na shughuli za vicoba ili kuwaepusha wananchi na maambukizi ya virusi vya corona.

Ametoa kauli hiyo leo Jumatano Machi 25, 2020 na kutaka kila mwananchi wilayani humo kuwa mlinzi wa mwenzake ili kujiepusha na maambukizi hayo.

Amesitisha sherehe ikiwemo harusi pamoja na matukio yote ya mikusanyiko.

''Nimepiga marufuku mikusanyiko yote kama vile viarano (makundi ya watu wanaokunywa mbege) ,sherehe zote, vikundi vya pesa (vikoba) na matukio yote ya mikusanyiko kwa wakati huu wa tahadhari ya corona mpaka nitakapotoa kibali.”

''Kila mwananchi awe mlinzi wa mwenzake kuhakikisha watu wote wanaotoka Kenya na nje ya wilaya ya Rombo wanafika katika vituo vya afya kupimwa afya zao kabla ya kuchanganyika na jamii,'' amesema Hokororo

No comments: