ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, March 25, 2020

TANZANIA YAPOKEA MSADA WA VIFAA TIBA KUKABILIANA NA JANGA LA CORONA

Maafisa wa Afya wa Tanzania wakipokea msada wa vifaa tiba vya kukabiliana na ugonjwa wa Corona kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Machi 24, 2020. 
Tanzania imepokea shehena ya vifaa tiba vya kukabiliana na ugonjwa wa Corona.
Vifaa hivyo ambavyo ni pamoja na barakoa (mask) 100,000, vifaa 20,000 vya kupima virusi vya Corona na mavazi maalum ya kujikinga 1,000, vimetolewa na bilionea wa China Bw. Jack Ma na taasisi yake ya Alibaba Foundation.
Kwa mujibu wa taarifa fupi iliyotolewa na ubalozi wa China hapa nchini leo asubuhi Machi 25, 2020 kupitiaas akaunti ya ubalozi huo @ChineseEmbtz imesema "Vifaa hivyo vinawakilisha utamaduni wa Wachina wa kushirikiana na China itatoa zaidi kwa Tanzania ili kusaidia mapbano dhidi ya maradhi ya Corona yanayosababishwa na kirusi cha COVID19.
Vifaa hivyo viliwasili Jumanne usiku Machi 24, 2020 na ndege ya Shirika la ndege la Ethiopia ambapo Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed ndiye anayeratibu misaada ya bilionea huyo aliyoitoa kukabiliana na janga la Corona katika nchi zote 54 za Afrika.
Aidha Waziri wa Afya Bi.Ummy Mwalimu kupitia akaunti take ya Twitter amemshukuru bilionea Jack Ma kwa msada huo na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed kwa kuwezesha shehena hiyo kufika nchini.

No comments: