ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, March 26, 2020

Wagonjwa wa Corona Wafikia 13 Tanzania

Image result for coronavirus
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amesema idadi ya wagonjwa walioambukizwa virusi vya Corona nchini imefikia 13 mpaka sasa.

Kwa mujibu wa maelezo yake, hadi Marchi 26, 2020, jumla ya watu 273, Tanzania bara (243) na Zanzibar (30) wamefanyiwa vipimo vya Corona, kati ya hizo sampuli 13 zilibainika kuwa na virusi vya Corona’ ambao kati yao 8 ni Watanzania na 5 ni wageni mikoa ikiwa:
– Arusha 2
– Dar 8
– Zanzibar 2
– Kagera 1
Wagonjwa 12 wote waliambukizwa nje ya nchi na mmoja aliambukizwa na mmojawao kati ya hao 12.

“Mgonjwa wetu wa kwanza ambaye haturuhusiwi kutaja jina lakini alijitaja mwenyewe amepona COVID 19, tumepima sampuli mara tatu na zote zimeonyesha negative, tumeanza utaratibu wa kumruhusu kurudi nyumbani,” amesema.

“Sasahivi tunaanza kutoa elimu ya kukataa unyanyapaa, kunyoosheana vidole, kulaumiana, Isabella amepona anatakiwa kurudi kwenye jamii na kupokewa bila kunyooshewa kidole,bila kudhalilishwa,bila kutukanwa,” Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.

No comments: