ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, March 26, 2020

Mgonjwa wa Kwanza wa Corona Tanzania Apona

ISABELA Mwampamba (46), mgonjwa wa kwanza kupatikana na virusi vya corona (COVID-19) nchini Tanzania, amepona na yupo huru kuungana na familia yake.

Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya amesema, muda wowote kuanzia sasa Isabela ataruhusiwa kuendelea na shughuli zake huku akitoa angalizo la kutonyanyapaliwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo tarehe 26 Machi 2020, Ummy amesema Isabela baada ya kupata vipimo vyote, vipimo vimeonesha kwamba yupo salama.

Tarehe 16 Machi 2020, Isabela alitangazwa kuwa mgonjwa wa kwanza kupatikana na virusi vya corona nchini, pia serikali ilianza ‘msako’ kwa wote waliokuwa karibu na Isabela ili kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo.

Pia Ummy ameseama mpaka sasa, Tanzania ina jumla ya wagonjwa 13 ambapo kati yao wanane ni Watanzania na watano ni wageni na kwamba Arusha (2), Dar es Salaam (8), Zanzibar (2) na Kagera (1).
Amesema, wagonjwa 12 wote waliambukizwa nje ya nchi na mmoja aliambukizwa na mmojawao kati ya hao 12.
GPL

No comments: