ANGALIA LIVE NEWS

Monday, April 27, 2020

Baada ya Kuugua Covid 19, Hatimaye Boris Kurejea Ofisini Leo


WAZIRI mkuu wa Uingereza Boris Johnson atarejea ofisini leo Jumatatu baada ya kupona maambukizi ya virusi vya corona.Msemaji wa serikali amelithibitishia shirika la habari la DPA.

Johnson alikuwa katika makazi yake yaliyoko nje ya London baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali ya Mtakatifu Thomas Aprili 12 alikolazwa kwa wiki nzima akitibiwa COVID-19.

Kulingana na shirika la habari la Uingereza la Press Association, siku ya Ijumaa Johnson alikutana na mawaziri waandamizi wa baraza lake kwa masaa matatu ikiwa ni pamoja na waziri wa mambo ya kigeni Dominic Raab aliyekaimu nafasi yake wakati akiwa mgonjwa.

Hata hivyo Johsnon anarejea katika wakati ambapo shinikizo linaongezeka dhidi ya serikali la miito ya kulegezwa vizuizi vya mapambano dhidi ya janga la corona.

No comments: