Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amepokea mchango wa sh. 100, 000,000/= Kutoka kampuni ya Taifa Gas kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali za kupambana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu - COVID-19. Pichani, Waziri Mkuu akiwa katika picha ya pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Makampuni ya Taifa, Abdulkarim Shah (kulia)
na Mkurugenzi Mtendaji wa Taifa Gas, Hamisi Ramadhani. Wa tatu kushoto ni Waziri wa Madini, Doto Biteko, wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile na kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanalı Said Matemwe. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya sh. 4, 000,000,000/= kutoka kwa Meneja Mkazi (Country Manager) wa Kampuni ya Madini ya Barric - Twiga Minerals, Hilaire Diarra (kushoto) na Msaidizi wake, Neema Ndossi (kulia) ukiwa ni mchango wa Kampuni hiyo kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali za mapambano dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu- COVID - 19. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Aprili 8, 2020. Wa pili kushoto ni Waziri wa madini, Doto Biteko na wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile. ( Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya Sh. 79,000,000/= ukiwa ni mchango wa ASASI za Kiraia wa kuunga mkono mapambano dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu- COVID-19 nchini. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Aprili 8, 2020. Pichani Kutoka kushoto ni Edward Mbogo, Mkurugenzi wa Idara ya Maafa , Ofisi ya Waziri Mkuu,Kanali Said Matemwe, Dkt. Stigmata Tenga, Lulu Ngw'anakilala, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile, Tike Mwambipile, Nasim Losai na kulia ni Brian Mosala. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea lita 50,000 za mafuta kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya mafuta ya Puma Energy Tanzania, Dominic Dhanah ( wa pili Kushoto) na Meneja Uzalishaji wa kampuni hiyo, Lameck Hiliyai (kulia) ukiwa ni mchango wa Kampuni hiyo wa kuunga mono mapambano dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu- COVID -19 nchini. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Aprili 8, 2020. Wa tatu Kushoto ni Waziri wa Madini, Doto Biteko, Wa pili Kulia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile na kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Maafa, ofisi ya Waziri Mkuu, Kanalı Said Matamwe. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wadau mbalimbali waliojitokeza kutoa michango kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za serkali za kupambana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu- COVID - 19 kwenye viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Aprili 8, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
No comments:
Post a Comment