Advertisements

Wednesday, April 1, 2020

Mfanyabiashara Azikwa na Benz Lake

MFANYABIASHARA maarufu nchini Afrika Kusini ameushangaza ulimwengu baada ya kuzikwa akiwa ndani ya gari lake aina ya Mercedes Benz ambalo ndilo lilikuwa gari alilolipenda zaidi kati ya magari yote aliyokuwa akimiliki.

Tshekedi Pitso ambaye pia alikuwa mwanachama wa United Democratic Movement (UDM) miaka miwili iliyopita aliiambia familia yake kuwa siku akifariki azikwe ndani ya gari lake hilo. Mfanyabiashara huyo alizikwa Jumamosi iliyopita katika Kijiji cha Jozana nchini humo akiwa kwenye pozi kama anaendesha gari hilo.

Pitso, alilinunua gari hilo miaka ya 1980s kwa gharama ya euro 500. Mpwa wake aitwaye Sefora (Pitso), 49, alisema familia imeshtushwa sana na msiba huo huku akiongeza kuwa Pitso alikuwa akisisitiza kuhusu namna mazishi yake yatakavyofanyika wakati atakapoondoka duniani.

Watu waliangalia kwa mshangao wakati Pitso, akiwa amevaa nguo zake nyeupe rangi ya maziwa na mikono yake ikiwa imeshika usukani huku gari hilo la Mercedes Benz likiteremshwa kaburini.


Maziko hayo yalikwenda sambamba na ujumbe mbalimbali kutoka kwa watu mashuhuri na chama chake cha UDM 
GPL

No comments: