Wednesday, April 8, 2020

MKURUGENZI WA JAMII FORUMS MAXENCE MELLO AKUTWA NA HATIA, MIKE MUSHI AACHIWA HURU

Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu jijini Dar es Salaam imemuhukumu Mkurugenzi wa Jamii Forums, Bw. Maxence Mello kulipa faini ya Shilingi Milioni 3 ama kwenda jela mwaka mmoja baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kuzuia Polisi kutekeleza majukumu yao.
Aidha mahakama hiyo imemuachia huru mshtakiwa mwenzake Bw. Mike Mushi baada ya kukosekana kwa ushahidi wa kutosha wa kumuhusisha na kosa. Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo Bw.Thomas Simba ndiye aliyetoa hukumu hiyo. Pichani chini Bw.Mello na mwenzake Mushi wakiwa kwenye mahakama hiyo leo Aprili 8, 2020 wakati na kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo.
Aidha Bw. Maxence Mello ameweza kulipa faini hiyo na kuachiwa huru.

No comments: