ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, June 20, 2020

Morrison arejea Yanga , aanza mazoezi


By THOMAS NG'ITU NA THOBIAS SEBASTIAN, Mwananspoti

WINGA wa Yanga, Benard Morrison ameungana tena na timu hiyo na jana amefanya mazoezi ya pamoja na wenzake yaliyofanyika katika uwanja wa Chuo cha Sheria, Dar es Salaam.

Morrison hakusafiri na kikosi kilichokwenda katika mikoa ya Shinyanga na Dodoma ambako kilicheza mechi za Ligi Kuu dhidi ya timu za Mwadui na JKT Tanzania kati

Winga huyo katika mazoezi hayo ya jana alionekana kuwa fiti kwa kufanya kila program ya mazoezi ambayo alikuwa akipewa na kocha Luc Eymael hadi mazoezi yalipomalizika.

Kocha Luc Eymael alisema urejeo wa nyota wake huyo ni mzuri huku akifurahishwa zaidi na kitendo chake cha kuomba msamaha kwa wenzake.

"Ni vizuri kurejea na aliomba msamaha katika bodi, wachezaji na hata mashabiki kwa hiyo ni jambo zuri kurejea katika kikosi," alisema Eymael.

Eymael alisema licha ya kurejea kwa Morrison, beki wake Said Makapu amepata majeraha madogo.

"Makapu kapata majeraha madogo tu kwenye mguu wake ndio maana nimeamua kumpumzisha, lakini wachezaji wengine wote wapo vizuri,” alisema.

Yanga baada ya kurejea juzi kutoka Dodoma ilikocheza dhidi ya JKT Tanzania, iliwapa mapumziko mafupi wachezaji wao na jana usiku wanaingia kambini kwenda kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Azam FC utakaopigwa Jumapili saa 10:00 katika Uwanja wa Taif

No comments: