Banda hilo lilizinduliwa rasmi juzi Jumamosi na mgeni rasmi akiwa ni nahodha wa timu hiyo, Papy Kabamba Tshishimbi, ambaye alitimba katika banda hilo kujionea historia ya klabu na kuzungumza na mamia ya mashabiki waliotembelea katika eneo hilo.
Mashabiki wa Yanga walipata nafasi ya kupiga picha na viongozi, baadhi ya makombe na medali zinazomilikiwa na klabu hiyo akiwemo Tshishimbi mwenyewe, kwa gharama ya shilingi 2,000 kwa kila picha moja.
Mbali na hivyo, wapo ambao walipata nafasi ya kujiunga na uanachama wa klabu hiyo, huku jezi zikipatikana kwa shilingi 15,000 na jarida la klabu hiyo likiuzwa pia katika banda hilo
chanzo:GPL
No comments:
Post a Comment