ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, July 8, 2020

Shilole ‘Alia’ na Kipigo Kutoka kwa Mumewe

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva na mjasiriamali, Zuwena Mohamed, maarufu kama Shilole, ameamua kuweka wazi matatizo ya ndoa yake kupitia ukurasa wake wa instagram. Shilole ambaye ni mke wa ndoa wa Ashrafu Sadiki maarufu kama ‘Uchebe’ ameeleza siri ya ‘Manyanyaso na Vipigo’ aliyokaa nayo kwa muda mrefu ndani ya ndoa yake.

Kupitia ukurasa wake wa instagram, Shilole amewaomba radhi Watanzania, hususan wanawake wenziye kwa kuificha siri hiyo kwa muda mrefu na kuwaaminisha kuwa ndoa yake haikuwa na tatizo lolote, wakati uhalisia wa mambo ni tofauti kabisa.

Katika post yake hiyo iliyowagusa sana Watanzania, Shilole ameambatanisha picha kadhaa zikimuonyesha akiwa na majeraha sehemu za usoni na kichwani, ambazo anadai ni baadhi ya picha za matukio tofauti ya unyanyasaji aliyowahi kuyapitia kutoka kwa Uchebe.

Mwisho wa post hiyo ameeleza kuwa amechoka kuvumilia mateso, na ameamua kuachana na ndoa hiyo na asitambulike tena kama mke wa Ashrafu ‘Uchebe’ na kuwaasa wanawake wenzie kutoficha unyanyasaji wanaokutana nao katika ndao zao.
Chanzo GPL

Na hikindio Shishi Baby alichoandika kwenye instagram yake
officialshilole
Verified

Naandika haya, nikiwa na akili timamu na utulivu, La kwanza kabisa nataka KUOMBA RADHI JAMII YANGU. Naomba radhi kwa sababu niliwaaminisha ndoa yangu haina tatizo, huku ukweli ukiwa hauko hivyo, nimekuwa mtu wa kuambulia vipigo na MENGINE yasiyozungumzika, Naomba radhi kwa sababu niliposikia wanawake wenzangu wakipigwa niliwaambia PAZENI SAUTI, niliposikia mwanamke kule Kigamboni ameuwawa na kuchomwa moto niliomboleza na jamii na kusema Bora angesema".. huku mimi nikijikausha na kujitoa kwenye kundi lao wakati ukweli wangu MIMI NI MWENZAO, Naomba radhi.
.
Mimi ni kioo cha jamii, tena sura kubwa ya wanawake. Leo numeona nivunje ukimya kwa kuweka wazi kwamba MUME WANGU ASHRAFU SADIKI, maarufu kama UCHEBE AMEKUWA ANANIPIGA SAAANA, na tena hata baada ya kunipiga hajali kupiga simu wala kujua naendeleaje, nauguzwa na watu baki hospitali, na bado manyanyaso mengine yanayoikosesha hii ninayoiita Ndoa uhai na furaha

na zaidi nina WATOTO, watoto wanaoniangalia kama Baba na Mama, leo nikubali kufa na kuacha wanangu barabarani, SITAWEZA
.
'Uchebe' ni mwanaume niliyempenda, nilimvumilia kwa madhaifu yote, nikampa kila kitu, (Utu wangu, Mali Zangu na hata palipotakiwa kumuendeleza asimame mwenyewe nilifanya kwakuwa nilijua tuko pamoja), lakini HILO HALIKUWAHI KUZUIA VIPIGO, DHARAU NA USALITI.
.
Siku 2 zilizopita baada ya kutoka SABASABA KUTAFUTIA WATOTO WANGU NA KUMTAFUTIA YEYE NILIPIGWA SANA. SABABU ZA KUPIGWA NI MIGOGORO MIDOGO YA KAWAIDA AMBAYO IPO KWENYE KILA NDOA, sio kwamba amenifumania au mambo yanayoshindwa kuzungumzika, hapana, Tena Namuheshimu sana, lakini solution aliyoiona ni kunipiga kinyama bila huruma, tena kwa kunishtua na ngumi nikiwa usingizini, Kama mnavyoona picha hapo ni matukio ya siku tofauti tofauti.

Najua nitalaumiwa kwa kuweka hili mtandaoni, ILA SINA NAMNA, MAISHA YANGU NI MAISHA YA WATU KWA KIASI KIKUBWA, JAMII INANITAZAMA KAMA MFANO.. Nimefika mwisho, na kuanzia sasa naomba nisitambulike kama Mke wa Uchebe, ila Mama alieamua kuweka maslahi ya watoto wake mbele na kuamua kuwa mwenyewe kwa usalama na furaha yake

Wakati nahangaikia mambo yangu ya ndoa, post hii itumike kuwakumbusha wanawake TUVUNJE UKIMYA, TUPINGE UKATILI, TUTAKUJA KUULIWA SABABU

No comments: