Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Abel Nyamahanga akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa ccm mkoa wa Iringa kuhusu utaratibu wa watia nia wa ngazi ya ubunge na udiwani mkoa Iringa
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Abel Nyamahanga akiwa na mjumbe wa halmashauri kuu (CCM) Taifa Salim Asas na katibu wa chama hicho wakizungumza na waandishi wa habari mkoani Iringa
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
KAMATI ya siasa ya chama cha
mapinduzi Ccm mkoa wa Iringa imewata watiania na wanachama kuheshimu kanuni na
sheria za uchaguzi zilizowekwa ndani ya chama ili kuepuka panga linaloweza
kujitokeza pindi watakapo kiuka taratibu za chama.
Mwenyekiti wa kamati ya siasa
Mkoa wa Iringa Abel Nyamahanga ameyasema hayo wakati akizungumza na wandishi wa
habari katika ukumbi wa ccm mkoa wa Iringa na kusema kuwa watia nia wanatakiwa
kupita ofisi za wasimamizi wa uchaguzi ili kupewa taratibu za uchaguzi.
Nyamahanga alisema chama
hakitasita kumchukulia hatua mwanachama na mtia nia ambaye atakiuka sheria na
taratibu za uchaguzi.
alisema kuwa kila kitu
kinachofanywa na chama cha mapinduzi kipo kwenye kanuni za uchaguzi za chama
hicho hivyo watia nia kwenye ngazi za udiwani na ubunge wanatakiwa kufuata
kanuni hizo ili waweze kutia nia bila kuwa na kashfa.
“Tunacho kizungumza hapa kila
kitu kipo kwenye miongozo na kanuni za chama chetu cha mapinduzi (CCM) ndio
maana tunawataka watia nia wote kufuta kanuni na taratibu za chama wakati wa
nia yake ya kutafuta nafasi ya kuwatumiakia wananchi” alisema Nyamahanga
Nyamahanga aliwataka wanachama
na watia nia wote kuheshimu kanuni za uchaguzi ndani ya chama cha mapinduzi ili
kuondokana na tatizo la rushwa ambalo miaka mingi kipindi cha uchaguzi ndio
huaribu taswiara ya chama cha mapinduzi.
Aidha Nyamahanga aliwataka
watia nia waache mara moja kupita kwenye kata na matawi kwa lengo la kukutana
au kuwasalimia wapiga kura badala yake wanatakiwa kupita katika ofis za
wasimamizi wa uchaguzi ili wapate taratibu na mwenendo wa uchaguzi unaokubarika
ndani wa chama hicho.
Alisema wapo baadhi ya watia nia wamekuwa
wakiwakusanya wapiga kura kutoa maeneo
mbalimbali kwa kisingio cha kuwasalimia,kujitambulisha na kuwapa nauli ikithibitika kwa mgombea
yoyote yule ataondolewa kwenye orodha ya wagombea kwa mujibu wa ibara ya 35
kifungu kidogo cha kumi na sita.
Kwa upande wake mjumbe wa
halmashauri kuu (CCM) Taifa Salim Asas alisema kuwa serikali ya chama cha mapinduzi
imeleta maendeleo kwa wananchi hivyo wanauhakika wa ushindi katika uchaguzi
mkuu.
Alisema kuwa chama cha
mapinduzi mkoa wa Iringa kitashinda kwa kishindo majimbo yote hata jimbo la
Iringa mjini ambalo lipo upinzani nalo watashinda kwa kuwa chama hicho
kimejipanga vilivyo kuhakikisha hakuna makundi ili kuhakikisha kwenye uchaguzi
mkuu wanaenda kwenye uchaguzi wakiwa wamoja.
Aliongeza kuwa wananchi wa
manispaa ya Iringa wamekuwa na imani na utendaji wa kazi wa chama cha mapinduzi
hivyo itakuwa kazi nyepesi kushinda kwa kuwa wanauhakika wa kumpata mgombea mwenye
uwezo wa kupeperusha pendera ya chama hicho.
No comments:
Post a Comment