Wednesday, July 22, 2020

Diamond, Parimatch watoa msaada kwa watoto wenye uhitaji



BEATRICE KAIZA

Staa wa Muziki wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul, ‘Diamond Platinum’ kwa kushirikiana na kampuni ya Parimatch Tanzania amewasaidia watoto yatima kwa kuwapa ‘Computer Generator’ na mahitaji muhimu ikiwamo chakula.
Akizungumza na Mtanzania Digital leo Jumanne Julai 21, jijini Dar Salaam Diamond amesema kuwa watu wengi hupenda kusaidia watoto yatima kwa kuwapatia chakula kwa siku moja lakini kwa upande wake ni tofauti na watu wanavyofanya kwani wao wamejipanga kutoa msaada kwa watoto hao mfululizo.
“Nguzo yetu ni kulinda na kujali kizazi cha baadae, tunaanza na idara ya elimu kwa kuwasaidia watoto wenye uhitaji kwa kuwapatia baadhi ya mahitaji muhimu.
“Naanza na vituo viwili vya makao ambavyo ni Huruma Islamic na Amani Foundation, vilivyopo jijini Dar es Salaam, tutawapa elimu pamoja na computer 10 ili waweze kuendana na kasi ya kisasa pamoja na genereta,” amesema Diamond Platnum.

Aidha ameongeza kuwa anatamani waunde timu ya mpira ambayo atasaidia kuwapa vifaa vya kuchezea mpira ikiwemo jezi, viatu, mpira kwa wachezeji kuchezea.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Parimatch, Tumaini Maligana amesema kuwa kampuni yao imejengwa katika misingi ya kusaidia jamii hususa katika nyanja za elimu, michezo na mazingira.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake