ANGALIA LIVE NEWS
Friday, July 10, 2020
Waliokutwa na kilo 1,378 za bangi washtakiwa
KULWA MZEE – DAR ES SALAAM , MTANZANIA
WAFANYABIASHARA waliokutwa na kilo 1,378.4 za bangi wameshtakiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi mkoani Arusha wakituhumiwa kujihusisha na biashara haramu ya dawa hizo.
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya iliwakamata watuhumiwa hao ambao walisomewa mashtaka jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha mbele ya Hakimu Mkazi, Gwantwa Mwankuga.
Upande wa Jamhuri uliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Seuri Kisambu maarufu Mollel na Losieku Mollel.
Washtakiwa wote wanashtakiwa kwa makosa ya kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya aina ya bangi kinyume na kifungu cha Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya sura ya 95 ya sheria za Tanzania.
Inadaiwa Juni 30, 2020 katika Kijiji cha Longilong, Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, Seuli alikutwa na kilo 649.5 za dawa za kulevya aina ya bangi na Losieku alikutwa na kilo 728.9 za dawa hizo.
Wa s h t a k i w a hawakuruhusiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka kisheria kusikiliza mashauri hayo ya uhujumu uchumi.
M a s h a u r i hayo yataendelea kutajwa kwenye mahakama hiyo yakisubiri utaratibu wa kuyapeleka Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu uchumi.
Kesi hiyo iliahirishwa hadi Julai 22 kwa kutajwa.
Wakati huo huo, Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imemkuta na kesi ya kujibu Said Malikita kwa kosa la kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.
Malikita anakabiliwa na kesi ya uhujumu Uchumi namba 12/2018.
Upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi nane huku mshtakiwa akitarajia kuwa na mashahidi wawili kwa utetezi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment