Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akipokea msaada wa Kompyuta 10 zenye thamani ya shilingi milioni 12 kutoka kwa Meneja wa Benki ya Azania mkoa wa Dodoma Makalla Mbura leo tarehe 10 Julai 2010. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Mary Makondo. Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza baada ya kupokea msaada wa Kompyuta kumi zenye thamani ya milioni 12 kutoka kwa Meneja wa Benki ya Azania mkoa wa Dodoma Makalla Mbura (Kulia) leo tarehe 10 Julai 2010. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Mary Makondo.Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi pamoja na Katibu Mkuu wake Mary Makondo wakisoma kijarida kinachoelezea masuala ya usajili wa hati alipotembelea ofisi ya Msajili wa Hati leo tarehe 10 Julai 2020 jijini Dodoma. (PICHA ZOTE NA MUNIR SHEMWETA WIZARA YA ARDHI)
Na Munir Shemweta, WANMM DODOMA
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amepokea msaada wa Kompyuta 10 zenye thamani ya milioni 12 kutoka Benki ya Azania.
Msaada huo ulipokelewa leo tarehe 10 Julai 2020 katika ofisi za ardhi mkoa wa Dodoma na kushuhudiwa na viongozi mbalimbali wa Wizara akiwemo Katibu Mkuu Mary Makondo.
Akizungumza baada ya kupokea msaada huo, Waziri Lukuvi aliishukuru Benki ya Azania kwa msaada huo alioueleza kuwa utasaidia sana kwenye huduma za sekta ya ardhi hasa katika ofisi za ardhi za mikoa zilizoanzishwa hivi karibuni.
Alisema, benki ya Azania imekuwa ikiunga mkono jitihada za Wizara kusaidia vifaa na kuzitaka taasisi nyingine kuiga mfano wa Benki ya Azania katika kusaidia juhudi za serikali kusogeza huduma za ardhi karibu na wananchi.
Kwa mujibu wa Lukuvi, hivi sasa wizara yake baada ya kuanzisha ofisi za ardhi katika mikoa inafanya jitihada mbalimbali kuhakikisha ofisi hizo zinakuwa na vifaa vya kutosha kwa lengo la kuwawezesha watendaji wa ofisi hizo kufanya kazi kwa ufanisi.
Kwa upande wake Meneja wa Benki ya Azania mkoa wa Dodoma Makalla Mbura alimueleza Waziri wa Ardhi kuwa msaada uliotolewa moja ya juhudi za benki hiyo kusaidia jitihada mbalimbali zinaziofanywa na wizara ya ardhi kwenye sekta ya ardhi.
Makalla aliongeza kwa kusema kuwa, benki hiyo itaendelea kuunga mkono jitihada za wizara katika masuala mbalimbali ya huduma za sekta ya ardhi kwa kutoa msaada pale unapohitajika.
No comments:
Post a Comment