ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, July 14, 2020

WAZIRI MWAKYEMBE ATEKELEZA AGIZO LA COSOTA KUHAMIA WIZARA YA HABARI UTAMADUNI SANAA NA MICHEZO

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe wakati akizungumza na wandishi wa habari leo jijini Dodoma wakati akitangaza kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli la kukihamisha Chama cha Haki Miliki (COSOTA) kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara kwenda Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo limeanza kutekelezwa rasmi leo.

Na. Alex Sonna, Dodoma

Agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli la kukihamisha Chama cha Haki Miliki (COSOTA) kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara kwenda Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo limeanza kutekelezwa rasmi leo.

Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe wakati akizungumza na wandishi wa habari leo jijini Dodoma.

Dkt. Mwakyembe amesema wamepokea kwa furaha uamuzi huo wa Rais Magufuli kwani unalenga kukuza na kuboresha maslahi ya wasanii nchini kutokana na shughuli zao za Sanaa.

Aidha Dk Mwakyembe ameweka wazi kuwa Rais Magufuli amesaini waraka wa kuhamisha COSOTA kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara kuja kwenye wizara anayoisimamia yeye.

Katika hatua hiyo Waziri Mwakyembe amemuelekeza Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa, Dk Hassan Abbas kukutana na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara ndani ya saa 24 kwa ajili ya kupeana makabidhiano pamoja na kutembelea Ofisi za COSOTA na kukutana na wadau wote wa Sana.

Dkt. Mwakyembe amesema kuwa Uamuzi wa Rais Magufuli ambao kwa hakika unalenga kuboresha maslahi ya wasanii nchini, kuihamishia COSOTA kwenye wizara yao kunaongeza urahisi zaidi wa kuwasaidia wasanii.

“Niwatake wenzangu ndani ya Wizara yetu kutambua tuna jukumu kubwa sana kulinda imani ya Rais wetu kwa kutuamini na kutupa fursa ya kumsaidia kusimamia kazi na hatimiliki za wasanii ambao yeye anawaamini na kuwapenda,” ametoa wito Dk Mwakyembe.

Amesema mara baada ya agizo la Rais Magufuli wameanza vikao ndani ya Wizara mara moja vya kujipanga kuangalia namna gani ya kupokea Cosota pamoja na kuweka utaratibu huku akimini ujio wa COSOTA wizarani hapo litakua ni tumaini kubwa kwa wasanii na wadau wa sanaa nchini.

No comments: