AFISA wa
Brela Nassoro Shomari Mtavu kulia
akikabidhi cheti cha jina la Biashara kwa mtumiaji huduma za wakala huo baada
ya kukamilisha taratibu za usajiliAfisa kutoka Brella
Bi Sada Kilabula kulia akiwapa maelezo wananchi waliotembelea banda lao
kwenye maonyesho ya nane nane mkoani Lindi
Team
ya Brela ikiongozwa na Mkurugenzi wa Utawala na Fedha Bakari Ally Mketo
wa pili kutoka kushoto wakiwa tayari Banadri kutoa huduma Afisa kutoka Brella Bi Sada Kilabula kulia akiwapa maelezo wananchi waliotembelea banda lao kwenye maonyesho ya nane nane mkoani Lindi
WAKALA wa usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imeshiriki maonyesho ya wakylima nane nane kwenye mikoa ya Simiyu na Lindi ili kuweza kuwafikia zaidi wananchi wake katika utoaji wa elimu ya kurasimisha biashara na huduma zinazotolewa na wakala huo.
BRELA
ni Taasisi iliyopo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara ambayo
jukumu la taasisi ni kusajili majina ya Biashara, makampuni, nembo za
huduma na biashara, Hataza, Utoaji wa leseni za Biashara daraja A na
Leseni za Viwanda.
Katika
Mkoa wa Lindi kwenye Maonyesho hayo wakala huo uliwakilishwa na
Mkurugenzi wa Utawala na fedha Bakari Mketo ambaye alibainisha kwamba
lengo kuu la kushiriki katika maonesho hayo ni kuhakikisha wananchi wote
wanapata huduma na utatuzi wa changamoto wanazokutana nazo wakati wa
kufanya sajili mbalimbali za BRELA papo kwa papo.
Pamoja na yote amewataka wakulima na wadau mbalimbali kuweza
kurasimisha biashara zao ili kutambulika na kuweza kuufikia Uchumi wa
kati.
Pia ameeleza kwamba dhumuni la kushiriki maonesho ni kuwasogezea
wananchi wa lindi huduma kwa ukaribu na kuendelea kutoa mafunzo juu ya
utumiaji wa mfumo wa usajili kwa njia ya mtandao.
Hata hivyo alitoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanatembelea katika
banda lao lililopo katika viwanja vya Ngongo ili kuweza kupata huduma za
sajili papo kwa papo.
No comments:
Post a Comment