Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Generali Wilbert A. Ibuge akizungumza na Balozi wa Ubelgiji hapa nchini, Mhe. Peter van Acker. Mazungumzo hayo ambayo yalifanyika kwa njia ya mtandao yalijikita kwenye kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Ubelgiji. Katika mazungumzo hayo, Balozi Ibuge aliishukuru Serikali ya Ubelgiji kupitia kwa Balozi huyo kwa ushirikiano mkubwa iliyoonesha kwa Tanzania katika mapambano dhidi ya janga la ugonjwa wa COVID-19 na ushirikiano katika miradi mbalimbali ikiwemo ya sekta ya maji kwenye baadhi ya mikoa hapa nchini. Mazungumzo hayo yalifanyika tarehe 28 Agosti 2020 huku Balozi Ibuge akiwa jijini Dodoma na Balozi Peter van Acker akiwa jijini Dar es Salaam
Balozi Ibuge akimsikiliza Balozi Peter van Acker wakati wa mazungumzo yao yaliyofanyika kwa njia ya mtandao.
Balozi Ibuge akiwa na ujumbe aliofutana nao wakati wa mazungumzo kati yake na Balozi wa Ubelgiji hapa nchini, Mhe. Peter van Acker (hayupo pichani). Kulia ni Bw. Hangi Mgaka, Katibu wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Bw. Anthony Mtafya, Afisa Mambo ya Nje
Kikao kikiendelea
No comments:
Post a Comment