By OLIPNA ASSA A OLIVER ALBERT
MSANII wa Bongo fleva, Konde Boy, ameibua shangwe kwenye Uwanja wa Mkapa baada ya kushuka uwanjani na kamba.
Msanii huyo aliyevalia mavazi yanayofanana nay a kijeshi alitumia kamba ndefu iliyofungwa juu ya uwanja na kuning'inia nayo katikati ya uwanja lakini ghafla ikaonekana kama inataka kukatika na hivyo kumpeleka chini na kisha kumrudisha juu kabla ya walinzi wake kwenda kumsaidia kumtoa.
Kabla ya Harmonize kuingia uwanjani walianza kuingia farasi watano, wanne waliwabeba askari na mmoja alimbeba shabiki mmoja aliyevalia jezi ya njano ya Yanga.
Kisha wakatoka watu 12 waliovalia nguo za kijani ambao walisimama sita kila upande na kuingia matarumbeta wakifuatiwa na wengine wanne waliongiawakiendesha baiske li na tisa wliovalia jez za njano.
Baada ya hapo wakaingia wadada 10 waliovalia suti za kaptura za njano na kufuatiwa na vijana wengine 10.
Baada ya dakika mbili kukapigwa wimbo wa tazama ramani utaona nchi nzuri Tanzania ambao ulionekana kuimbwa na mashabiki wote.
Harmonize alianza kuimba wimbo wake mpya wa Jeshi na baadae kusalimia mashabiki na kuanza kuimba wimbo wa Yanga ulioteka hisia mashabiki walioimba nae pamoja.
No comments:
Post a Comment