ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, August 5, 2020

Mlipuko Waua 78, Waharibu Majengo Beirut

LEBANON inaomboleza baada ya mlipuko mkubwa katika mji mkuu wa Beirut kuwaua watu 78 na kuwajeruhi wengine 4000 jana (Jumanne).
Mji wote uliyumbishwa na mlipuko huo, ulioanza kwa moto katika bandari kabla mlipuko huo uliofanana na wingu la uyoga kutokea.
Rais Michel Aoun alisema kwamba tani 2,750 za ammonium nitrate zilikuwa zimewekwa vibaya katika ghala moja kwa miaka sita.
Aliitisha kikao cha dharura siku ya Jumatano na kusema hali ya dharura ya wiki mbili imetangazwa.
Aoun pia alitangaza kwamba serikali itatoa Dola mil. 66 za hazina ya dharura.
”Kile tunachoshuhudia ni janga kubwa’,’ alisema mkuu wa kundi la Msalaba Mwekundu, George Kettani, akizungumza na vyombo vya habari na kuongeza: ”Kuna waathiriwa kila mahali

No comments: