Sunday, August 9, 2020

NMB YAWAHAKIKISHIA WAKULIMA KUWAUNGA MKONO

Katika maadhimisho ya Nane Nane kitaifa yaliyofanyika viwanja vya Nyakabindi Mkoa wa Simiyu, Benki ya NMB imewahakikishia wakulima kuwa wako nao pamoja ili kuhakikisha wanasonga mbele zaidi. Hata hivyo benki hiyo imepata fursa kubadilishana uzoefu na wakulima- namna nzuri ya kukuza kilimo chao na pia kuweza kuona fursa zilizopo.

Akielezea ni namna gani Benki hiyo inaunga mkono juhudi za serikali, Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara – Filbet Mponzi alisema “Mchango wetu kama benki wakujenga Uchumi imara kupitia kilimo na ufugaji ni kuwa kwa mwaka huu, tumetoa zaidi ya TZS Bilioni 230 kama mikopo kwenye mazao ya Pamba, Korosho Kahawa, Katani, Tumbaku, Mihogo, Mchele na Mahindi”.Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB- Filbert Mponzi ni jinsi gani benki hiyo inawezesha sekta wa kilimo nchini, alipotembelea banda la benki hiyo kwenye maonesho ya Nane Nane katika viwanja vya nyakabindi Mkoa wa Simiyu.

Ndani ya miaka miwili, NMB imefungua akaunti zaidi ya 600,000 za wakulima. Mponzi aliongeza kuwa “hadi leo kwenye mabanda yetu yote ya Nane Nane nchi nzima ambapo tumeshiriki; Kanda ya Nyanda za juu, Kanda ya kaskazini, Magharibi, Kanda ya Ziwa, Kusini na Kanda ya Kati tumeweza kufanya mafunzo kwa viongozi wa wakulima jumla 52,700 ambao pia wameweza kuwanufaisha wenzao 141,060.
Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB- Filbert Mponzi, Mkuu wa Kitengo cha Biashara za Serikali wa Benki ya NMB – Vicky Bishubo na Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi- Sosthenis Magesse katika picha ya pamoja na Maafisa wa Benki hiyo kwenye banda lao la maonesho ya Nane Nane katika viwanja vya nyakabindi Mkoa wa Simiyu.

Pia, Kwa mwaka huu, NMB Imetenga TZS 1.9 billioni kwaajili ya ujenzi wa maghala (warehouse) kuhifadhi mazao ya wakulima. Aidha, kupitia ‘NMB Foundation’ NMB imeweza kutoa elimu ya fedha na mafunzo ya biashara kwa vyama vya ushirika wa wakulima (AMCOS) 1550 nchi nzima, ili kuwajengea uwezo wa namna bora ya kusimamia mapato yao. Kwa Kanda ya Mashariki ya Ziwa (Shinyanga, Mara na Simiyu) wameweza kufikia AMCOs zaidi ya 700.

Tangu 2016, NMB imetoa zaidi ya TZS 800 bilioni kusaidia kilimo na mnyororo wa thamani wa mazao ya kilimo

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake