ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, August 23, 2020

RC HAPI AWAPONGEZA SAO HILL KWA KUJENGA LA BWENI KWA GHARAMA YA ZAIDI YA MILIONI 114 KATIKA SHULE YA CHANGALAWE

Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi amewapongeza TFS shamba la miti la Sao Hill kwa kujenga la bweni la shule ya sekondari ya Changalawe kwa kutumia zaidi ya milioni 114 iliyopo Mafinga Mjini katika wilayani ya mufindi .
Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akiwa na mkuu wa shule ya sekondari ya Changarawe wakati wa kukagua ujenzi wa bweni lilofadhiliwa na Sao Hill
Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akiwa na mkuu wa shule ya sekondari ya Changarawe wakati wa kukagua ujenzi wa bweni lilofadhiliwa na Sao Hill

NA FREDY MGUNDA,MUFINDI.

Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi amewapongeza TFS shamba la miti la Sao Hill kwa kujenga la bweni la shule ya sekondari ya Changalawe kwa kutumia zaidi ya milioni 114 iliyopo Mafinga Mjini katika wilayani ya mufindi na kuwaomba wadau wengi wajitolee kama ambavyo Sao hill walivyofanya

Hayo yamesemwa mara baada ya ukaguzi wa bweni la wanafunzi wa kike katika shule ya sekondari Changalawe wilayan Mufindi lililojengwa na Wakala wa misitu Tanzania TFS kupitia shamba la miti Sao hill lililogharibu zaidi ya sh. Milioni 114.

Akizungumza na wafanyakazi na wanafunzi wa shule hiyo,Hapi alisema kuwa jingo la bweni alilololikagua ameridhika nalo kutokana na thamani ya fedha kutumika kikamilifu kwa kuzingatia ushauri wa kitaalamu kutoka kwa wadau wa serikali ndio maana jingo hilo limejengwa kwa viwango stahili.

Hapi aliwataka walimu kuendelea kutoa elimu bora kwa wanafunzi wa shule hiyo ili kuzalisha kizazi cha wasomi wenye maarifa ya darasani na maisha kwa ujumla kwa kuwa shule hiyo imekuwa ikifanya vizuri kiwilaya,mkoa na taifa kwa ujumla.

Katika risala ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga Saada Mwaruka iliyosomwa na mkuu wa shule ya Sekondari Changarawe imebainisha kuwa ufadhiri huo utasaidia jumla ya wanafunzi 80 kukaa shuleni hapo na kuondokana na hatari ya kukatisha masomo kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo tatizo la mimba kwa wanafunzi.

Alieleza namna Jitihada zake za kuandika miradi ya utatuzi wa changamoto za shule ulivyosaidia kuwavutia wafadhiri hao ambao Sao Hill hadi kufanikisha upatikanaji wa majengo kadhaa ikiwemo bweni hilo.

Hatua hii imeonesha kumpendeza mkuu wa Mkoa Ally hapi licha ya kuwataka viongozi wengine wa taasisi za serikali ikiwemo shule kujenga utamaduni wa kuandika miradi yenye kuomba ufadhiri kwa wadau ametoa maagizo kwa wakuu wa wilaya zinazokutikana wilani huo

Kando ya hayo awali katika ziara hiyo mkuu wa mkoa amefanya uzinduzi wa jengo la maabara katika zahanati ya Rungemba wilayani humo…na kuahidi kukabidhi mifuko 100 ya saruji ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za wananchi hao waliojitoa kuchangia na kukamilisha ujenzi wa maabara hiyo.

Maeneo mengine yalifikiwa na mkuu wa mkoa katika ziara hiyo iliyobatizwa jina la Iringa mpya ni pamoja na hospitali ya halmashauri ya Mji wa Mafinga pamoja na eneo la ofisi za shamba la miti sao hill ambapo amepokea mtambo wa kisasa wa kuzimia moto ulionunuliwa na Serikali na kisha .

No comments: