Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi akizungumza wakati wa kufungua mkutano wa 17 wa siku ya Wahandisi mkutano ulioenda sambamba na kiapo kwa wahandisi wapya katika kutumikia taaluma zao uliofanyika leo jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi akisisitiza jambo kwa washiriki wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 17 wa siku ya Wahandisi mkutano ulioenda sambamba na kiapo kwa wahandisi wapya katika kutumikia taaluma zao uliofanyika leo jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya
Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga,akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa 17 wa siku ya Wahandisi mkutano ulioenda sambamba na kiapo kwa wahandisi wapya katika kutumikia taaluma zao uliofanyika leo jijini Dodoma.
mwenyekiti wa bodi ya usajili wa Wahandisi nchini (ERB) Prof. Ninatubu Lema, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 17 wa siku ya Wahandisi mkutano ulioenda sambamba na kiapo kwa wahandisi wapya katika kutumikia taaluma zao uliofanyika leo jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Binilith Mahenge,akitoa taarifa ya Mkoa wake kwenye Mkutano Mkuu wa 17 wa siku ya Wahandisi mkutano ulioenda sambamba na kiapo kwa wahandisi wapya katika kutumikia taaluma zao uliofanyika leo jijini Dodoma.
Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi, Patrick Barozi,akitoa taarifa kweye ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 17 wa siku ya Wahandisi mkutano ulioenda sambamba na kiapo kwa wahandisi wapya katika kutumikia taaluma zao uliofanyika leo jijini Dodoma.
Sehemu ya Wahandisi 400 wakila kiapo cha utii kwenye Mkutano Mkuu wa 17 wa Wahandisi uliofanyika leo jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi akiwa katika picha za pamoja mara baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa 17 wa siku ya Wahandisi mkutano ulioenda sambamba na kiapo kwa wahandisi wapya katika kutumikia taaluma zao uliofanyika leo jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna,Dodoma
Serikali imeitaka bodi ya usajili wa Wahandisi nchini (ERB) kuwachukulia hatua Wahandisi wanaokwenda kinyume na taaluma zao na kufuata matakwa yao binafsi katika kutekeleza majukumu yao.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dodoma na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi wakati akifungua mkutano wa 17 wa siku ya Wahandisi mkutano ulioenda sambamba na kiapo kwa wahandisi wapya katika kutumikia taaluma zao.
Balozi Kijazi amesema kuwa Uhandisi ni Taaluma muhimu na wanataaluma wanatakiwa kuiheshimu na bodi ya usajili ihakikishe inawachukulia hatua kali za kisheria wanaokiuka miiko yao kwa sababu wameapa kufuata masharti ya taaluma.
” Bodi isisite kuwachukulia hatua kali wale wanaoenda kinyume kweli ninyi ni walezi lakini hakikisheni wahandisi wanafuata masharti na wanaokiuka mnawachukulia hatua kali” amesema balozi Kijazi.
Hata hivyo Balozi Kijazi amewataka wataalamu hao kutumia taaluma yao kikamilifu na kuanzisha mifumo ya ndani ili kama nchi tusitegemee mifumo ya nje ya nchi na tutumie mifumo yetu wenyewe.
Amesema Serikali ya awamu ya tano inatekeleza miradi mikubwa ya kimkakati ili kufikia nchi ya viwanda mfano mradi wa mwalimu Nyerere wa kuzalisha umeme ambao utazalisha umeme mwingi utakao wezesha katika kuendesha viwanda.
” Ninyi kama wahandisi mtumie fulsa hii ya mapinduzi ya viwanda kwa sababu taaluma hiyo itahitajika Sana hasa katika ujenzi na uendeshaji wa Viwanda hivyo na tutakuwa na umeme wa kutosha kuendesha viwanda hivyo” amesema. Balozi Kijazi
Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya usajili wa Wahandisi nchini (ERB) Prof. Ninatubu Lema, amesema mkutano huo ni wa siku mbili kwa wahandisi kujadili changamoto zinazowapata katika utekelezaji wa majukumu yao.
Amesema katika mkutano huo wahandisi takribani 452 wataapa kiapo kwa ajili ya kuheshimu taaluma hiyo katika utekelezaji wa majukumu yao katika taaluma hiyo.
Amebainisha kuwa mpaka Sasa bodi hiyo imesajili wahandisi elfu ishirini na tisa(29) na malengo yao kusajili wahandisi elfu themanini (80) ifikapo 2025.
No comments:
Post a Comment