Wednesday, September 16, 2020

CHUMI: MAFINGA KUFANYABIASHARA MASAA 24 KAMA AKIWA MBUNGE WA JIMBO LA MAFINGA MJINI

Mgombea ubunge katika jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi akiomba kura wananchi wa mtaa wa Lumwago
Mgombea ubunge katika jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi akiwa kwenye mkutano wa kampeni

Na Fredy Mgunda,Mafinga.

MGOMBEA ubunge katika jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi kuendelea kuiomba serikali kuruhusu wananchi kufanya biashara masaa ishirini na manne Kama ilivyo katika kusafirisha mazao ya misitu.

Akizungumza kwenye mkutano wa wa kuomba kura kwa wananchi wa mtaa wa Lumwago,Chumi alisema kuwa ilikukuza uchumi kwa wananchi wa jimbo la Mafinga Mjini wanatakiwa kufanya shughuli za kimaendeleo kwa masaa yote ishirini na nne.

Chumi ambaye anayetetea nafasi yake, amesema kama ambavyo Serikali ilikubali kuruhusu malori kusafiri masaa ishirini na manne anaamini Serikali itaridhia wananchi wa Mafinga wafanye biashara masaa 24.

“Huu ni Mji wa kibiashara, sio Saa nne tu polisi hawa hapa wanataka ufunge biashara, haiwezekani, nitaongoza hoja ya kubadilisha sheria Watu wajiachie wafanye biashara usiku na mchana”alisema Chumi

Alisema Wananchi wa Mafinga wana bidii ya kufanya kazi, kufanya biashara masaa ishirini na manne itaongeza kipato cha mtu mmoja mmoja, Halmashauri na Taifa kwa ujumla.

Aidha Chumi alisema wafanyabiashara wanatakiwa kufanyabiashara muda wowote ili kuongeza kipato chao kama ilivyokuwa kwenye nchi zilizondelea hasa kwenye miji midogo inayokuwa kiuchumi

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake