Tuesday, September 15, 2020
MGOMBEA UBUNGE ACT AAHIDI KULINDA HAKI ZA WAVUVI
NA AVELINA KITOMARY
MGOMBEA Ubunge anayepewa nafasi kubwa ya kushinda nafasi ya ubunge Jimbo la Kigamboni Kwa tiketi ya Chama cha Act _wazalendo Mwanaisha Mndeme amewaomba wananchi wa Kigamboni wamchague ili awe mbunge wa Jimbo hili huku akihaidi kulinda Haki za wavuvi Wilayani humo.
Kwa miaka zaidi ya kumi Sasa Jimbo hilo limekuwa Chini ya chama cha Mapinduzi CCM lakini hadi leo vijana wa kigamboni karibu asilimia 79 hawana ajira rasmi na wanajihusisha na shughuli haramu ikiwa biashara ya ngono, uuzaji na utumiaji wa madawa ya kulevya.
Mwanaisha ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara ambao umefanyika katika viwanja vya Tungi Mnadani Kigamboni jijini Dar es salaam.
Ameendelea kwa kusema endapo wananchi wakigamboni wakinichagua hatua ya Kwanza nitashughulikia changamoto za wavuvi.
“Nawaomba ndugu zangu mnichague kwani shida zenu nazijua na ni za miaka mingi sekta ya uvuvi .ukosefu wa ajira Kwa vijana ,mikopo Kwa akina ,ukosefu wa huduma Bora za Afya .haya yote mkinichagua nitakwenda kuyashughulikia.”amesema Mwanaisha
Ameongeza kuwa kigamboni kunachangamoto ya makazi Bora hivyo Kama watamchagua atatumia elimu yake ya uwanasheria na kushirikiana na watu wa mipangomiji, na mazingira kuhakikisha wanapima Ardhi ili wananchi wapate fursa ya kukopesheka.
Amesema kuwa miaka kumi ya mbunge aliyemaliza muda wake ni miaka ya changamoto nyingi Kwa wananchi wa Kigamboni na ndio maana hata yeye mwenyewe anakiri huku aliwataka ninyi wananchi mumchague tena ili akamalizie kazi .nakwamba wamkatae kwani hatoshi.
“Ndugu zangu Mimi ni biti mdogo lakini ni mwanasheria nawahakikishia mkinipa kura nakwenda kufanya mambo makubwa Kwa ajili ya Kigamboni yetu .si mnajua changamoto za Afya zilivyo madawa tatizo,lakini upande wa elimu madarasa machache katika shule zetu nitahakikisha mkinichagua tunakwenda kumaliza kero hii.”amesema
Amefafanua kuwa katika Halmashauri kuna mikopo asilimia kumi inatoka katika makundi matatu ya vijana,akina mama,na walemavu asilimia Mbili wakimchagua atakwenda kuwambania ili nawenyewe wanufaiki nayo tofauti na ilivyo sasa ambapo wachache ndio wanafaidika.
Pia amezungumzia kuhusu soko kwamba Wilaya ya Kigamboni Kwa muda mrefu imekosa soko la uhakika hali inayowalazimu wananchi kufuata huduma nje ya Kigamboni wakati maeneo ya wazi hapo hivyo wakimchagua atashughulikia kero hiyo ambayo ki kubwa Kwa wananchi hao.
Alimaliza Kwa kuwaomba wananchi hao ili mambo yaende vizuri Basi wahakikishe wanampa kura Diwani anayotokana na Chama hicho Ally Sharif pamoja na mgombea urais Bernard Membe.ifikapo mwezi Oktaba 28 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake