Mgombea wa ubunge jimbo la Iringa Mjini kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) mchungaji Peter Msigwa akiwa kwenye mkutano wa kampeni kata ya Ruaha mkoani Iringa
Baadhi wananchi waliojitokeza kumsikiliza Mgombea wa ubunge jimbo la Iringa Mjini kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) mchungaji Peter Msigwa akiomba kupewa ridhaa ya kuwa mbunge tena
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Mgombea wa ubunge jimbo la Iringa Mjini kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) mchungaji Peter Msigwa amewahakikisha wapiga kura kuwa hakutakuwa na diwani wa la mbunge atakayekihama chama hicho kwa kuwa wameteu viongozi wanaokipenda chama hicho kuliko mwaka 2015.
Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni katika kata ya Ruaha,Msigwa alisema kuwa baadhi ya madiwa walihamia CCM kwa ajili ya uroho wa fedha na madaraka na walikuwa hawana nia njema ya kuwatumikia wananchi katika kata zao.
Msigwa alisema kuwa wagombea wa udiwani katika uchaguzi wa mwaka huu wamewateua wagombea ambao ni viongozi kweli kweli na wenye nia njema ya kuwatumikia wananchi katika kuwaletea maendeleo.
Msigwa aliwaomba wananchi wa kata ya Ruaha kupigia kura mgombea wa ubunge, udiwani na urais wa CHADEMA kwa kuwa hao ndio viongozi bora katika uchaguzi wa mwaka huu.
Aliwakumbusha wananchi wa kata ya Ruaha kukichagua chama cha maendeleo na demokrasia (CHADEMA) kwa kuwa ndio chama ambacho kimesaidia kuleta maendeleo yanayoonekana hivi sasa kwenye kata hiyo.
Aidha Msigwa aliwaomba wananchi kuwapigia kura kwa wingi wagombea wa CHADEMA ngazi zote kwa kuwa chama hicho kimejipanga vilivyo kuzilinda kura za wananchi hao zisiibiwe na wapinzani wao.
Kwa upande wake mgombea wa udiwani kata ya Ruaha kupitia cha chama maendeleo demokrasia na maendeleo CHADEMA Patrick Nyaulingo alisema kuwa wananchi wanapaswa kuchagua wagombea wa CHADEMA kwa ajili ya kupata maendeleo ya uhakika
No comments:
Post a Comment