Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limeagiza mitambo mitatu ya uchorongaji yenye teknolojia na ya kisasa zaidi kuwahi kutumika hapa nchini. Moja wa mtambo huu unauwezo wa kuendeshwa kwa kutumia computer na mtu akiwa mbali na mashine.
Tukio hili la uziduzi limefanyika leo kwa kudhihirishia umma wa Tanzania, kuwa Shirika limethubutu na limedhamiria kuleta mapinduzi katika soko la madini kwa kuingia kwa nguvu zote kwenye shughuli za uchorongaji.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa mitambo hiyo, Katibu Mkuu Wizara ya Madini Profesa Simon Msanjila ameipongeza STAMICO kwa hatua kubwa waliofikia na uthubutu wa kuleta ushindani katika soko la uchorongaji amewataka watumishi kuendelea kufanya kazi kwa bidi ili kuleta tija na maendeleo kwa Taifa.
Akiongea kuhusu mitambo hiyo, Mkurugezi wa STAMICO, Dkt. Venance Mwasse amesema ni jambo la kujivunia sana kununua mitambo hiyo ya kisasa.
“Tumeagiza mitambo hii mitatu ya kisasa kabisa na mmoja kati ya huo mtambo ni Explorac 235 wenye uwezo wa kuchimba hadi mita 500 kwa siku. Mtambo huu ni mpya na kiteknolojia yake ni ya hali ya juu na hakuna kampuni nyingine ambayo imeshawahi kutumia matambo hapa nchini. STAMICO ndio shirika la kwanza kuwa na mtambo kama huu.

Dkt. Mwasse ameishukuru Wizara ya Madini kwa maelekezo na ushirikiano unaoendelea kutolewa kwa STAMICO na kutoa rai kwa wadau wadau wa uchorongaji kufanya kazi na STAMICO. Mitambo hii inategemea kusafirishwa Kwenda maeneo mbali mbali tayari kuanza kazi ya uchorogaji mara moja
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake