Thursday, September 17, 2020

MSIGWA AAHIDI NEEMA JIMBO LA IRINGA MJINI KAMA AKIPEWA RIDHAA YA KUWA MBUNGE TENA


Mgombea ubunge wa jimbo la Iringa Mjini kupitia chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA Mchungaji Peter Msigwa akiwamkutanoni

Na Fredy Mgunda,Iringa.

Mgombea ubunge wa jimbo la Iringa Mjini kupitia chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA Mchungaji Peter Msigwa amewaomba wananchi wa jimbo hilo kumpa miaka mitano mingine ili aendelee kuleta maendeleo kama alivyofanya kwenye miaka kumi ya ubunge wake.

Akizungumza kwenye mkutano wa kuomba kura kwa wananchi wa kata ya Igumbilo Msigwa alisema kuwa Iringa ya sasa imepiga hatua kimaendeleo baada ya kufanya kazi kubwa ya kimaendeleo kama kuboresha sekta ya afya na miundombinu.

Alisema kuwa barabara nyingi za jimbo la Iringa Mjini zimejengwa kwa kiwango cha lami kutokana na juhudi za kujenga hoja bungeni na kwa wadau mbalimbali ambao walisaidia kujenga barabara hizo.

“Mnakumbuka ninapoingia madarakani asilimia kubwa barabara zetu zilikuwa za vumbi hivyo nilijitahidi kupambana kuhakikisha kuwa Iringa Mjini inakuwa na miundombinu bora ya barabara”alisema Msigwa

Msigwa aliongeza kwa kusema kuwa wamefanikiwa kuboresha sekta ya afya tofauti na ilivyokuwa awali na ameahidi kuboresha sekta ya afya kwa kutoa bima za afya kwa wananchi wote kwa kuwa ndio Sera ya CHADEMA katika uchaguzi wa mwaka huu.

Lakini Msigwa alisema kuwa ni aibu kwa wananchi wa jimbo la Iringa Mjini kushindanisha na mgombea wa chama cha mapinduzi (CCM) Jesca Msambatavangu kwa kuwa hata uwezo wa kuliongoza jimbo la Iringa Mjini.

Msigwa alimalizia kwa kuwaomba wananchi wa jimbo la Iringa Mjini kupigia kura mgombea urais wa CHADEMA Tundu Lisu na diwani wa CHADEMA kata ya Igumbilo kwa maendeleo ya nchi,jimbo na kata hiyo.

Kwa upande wake mgombea wa udiwani kata ya Igumbilo kupitia chama cha demokrasi na maendeleo CHADEMA…..alisema kuwa anahakikisha anatatua changamoto ya mabweni,zahanati,barabara,vivuko mbalimbali viwanja vya michezo na tatizo la maji kwenye baadhi ya mitaa

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake