Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce K. Nzuki akiipongeza UNDP kwa msaada waliotoa kutengeneza magari yatakayotumika kubeba watalii pindi watakapopatwa na dharura za maradhi, wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya magari hayo iliyofanyika kwenye ofisi za Hanspaul, Jijini Arusha.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce K. Nzuki akikata utepe pamoja na Muwakilishi Mkazi wa UNDP Tanzania Bi. Christine Musisi pamoja na viongozi wengine, wakati wa hafla ya makabidhiano ya magari ya dharura (ambulance) iliyofanyika katika ofisi za Hanspaul, Jijini Arusha.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce K. Nzuki akiwa ndani ya gari la dharura (ambulence) mara baada ya hafla fupi ya makabidhiano ya magari hayo yatakayo hudumia watalii, Jijini Arusha.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce K. Nzuki akiwa ameambatana na Muwakilishi Mkazi wa UNDP Tanzania Bi. Christine Musisi (katikati) pamoja na moja ya wakurugenzi wa kampuni ya Hanspaul, Bw. Satbir Singh Hanspaul wakati wa hafla fupi ya Makabidhiano wa magari manne ya dharura yaliyotolewa na Chama cha Makala wa Utalii Tanzania (TATO), Jijini Arusha.
Kauli hiyo imetolewa Jijini Arusha na Katibu Mkuu Wizara ya Malisiali na Utalii Dkt. Aloyce K. Nzuki wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika Warsha ya kupokea maoni ya wadau wa utalii katika kuandaa mkakati wa kurejesha sekta ya utalii katika hali yake ya awali baada ya mapambano dhidi ya COVID-19.
‘’Tulitengeneza Mkakati huo ambao unaitwa Standard Oparate Procedures ili kuhakikisha kwamba tunaishi na ugonjwa huu kwa maana ya kwamba tusisimamishe shughuli za kuwapokea watalii lakini tujue namna ya kuwapokea watalii ili kusudi watalii wawe salama na watoa huduma wawe salama’’ amesema
Katika Mkakati huo amesema waliahidi kwamba katika maeneo yao ya utalii wataweka magari ya kubebea wagonjwa ikiwa ni pamoja na kuandaa maeneo ambayo yatasaidia kutoa huduma pale ambapo ikitokea watalii wamepata tatizo ama watoa huduma wamepata tatizo waweze kuhudumiwa katika vituo vya kutolea huduma za Afya.
Wakati huo huo amelishukuru Shirika la UNDP kwa kushiriki kuandaa na kuboresha magari ya kubebea wagonjwa kwa kuyabadilisha magari hayo kutoka magari ya kawaida na kuwa magari ya kubebea wagonjwa ambayo yatasaidia kuhudumia watalii watakaopata dharura za maradhi pindi wakiwa katika ziara zao.
‘’Tunalishukuru Shirika la hili la UNDP limefadhili pamoja na kugharamia magari hayo. Tunashukuru sana kwa kutusaidia na sasa wanatusaidia kazi nyingine maarufu na muhimu sana ambayo ni ya kutengeneza mkakati wa kurejesha hali ya utalii kama ilivyo kuwa awali’’
No comments:
Post a Comment