Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera ,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC Njedengwa jijini Dodoma wakati akitoa ufafanuzi kuhusu upotoshwaji unaofanywa na baadhi ya viongozi wa vyama kutangaza kuwa kuna vituo hewa vya kupigia kura nchini vimeongezwa.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifatilia hotuba ya Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera ,alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu upotoshwaji unaofanywa na baadhi ya viongozi wa vyama kutangaza kuwa kuna vituo hewa vya kupigia kura nchini vimeongezwa katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC Njedengwa jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera ,akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC Njedengwa jijini Dodoma wakati akitoa ufafanuzi kuhusu upotoshwaji unaofanywa na baadhi ya viongozi wa vyama kutangaza kuwa kuna vituo hewa vya kupigia kura nchini vimeongezwa.
Na.Alex Sonna,Dodoma
Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchin (NEC) imekanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa kuna vituo hewa vya kupigia kura vimeongezwa katika baadhi ya majimbo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera,amesema kuwa hakuna vituo hewa vya kupigia kura nchini huu ni upotoshwaji unaofanywa na baadhi ya viongozi wa siasa kutangaza kuwa kuna vituo hewa.
”Nashangaa kuona taarifa za uzushi zikisambaa kwenye mitandao na baadhi ya viongozi wa vyama kuanza kulalamika na kuzusha kuwa NEC imeongeza vituo hewa vya kupigia kura nchini”amesema Dkt.Mahera
Aidha, amesema vituo vya kupigia kura ni vingi kuliko vya kujiandikishia kwa sababu kila kituo wameweka idadi ya wapigakura wasiopungua 500 ili kurahisisha zoezi la upigaji kura.
“Vituo vilivyotumika kuandikisha wapiga kura vilikuwa 37,814,na vituo vya kupigia kura ni 80,155, hii inatokana na kwamba kwenye kituo kimoja kilichotumika kujiandikisha kinaweza kutoa vituo vitatu kwa sababu kituo kimoja kinatakiwa kuwa na wapiga kura 450 hadi 500,” amesema Dkt.Mahera.
Hata hivyo amewataka wagombea wa kiti cha Urais na Makamu wa Rais kuzingatia ratiba toleo la sita ya kampeni iliyotolewa na Tume.
Dkt.Mahera amesema kuwa Tume imejiandaa vizuri katika uchaguzi huo na kuwa tayari vifaa vyote muhimu leo vitakuwa vimefika kwenye majimbo ya Tanzania bara na Zanzibar.
“Pia Tume inawataka wasimamizi wa majikbo wafikishe kuanzia leo vifaa kwenye vituo vya kupigia kura ili kusijitokeze dosari zozote kwenye uchaguzi ikiwemo kuchelewa kwa vifaa na kufunguliwa vituo,”amesema.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake