Saturday, October 10, 2020

MKUU WA MKOA ATOA ONYO KWA WAFUGAJI KOROFI PWANI

Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evaristi Ndikilo ametoa onyo kali kwa wafugaji wa Mkoa wa Pwani kutoharibu mazao ya wakulima na kusisitiza kuwa serikali haitasita kumchukulia hatua za kisheria mfugaji yeyote atakayekiuka amri hiyo.

Mhandisi Ndikilo ametoa onyo hilo Jumamosi Oktoba 10, 2020 alipokuwa akitembelea maeneo mbalimbali ya kilimo katika bonde la Ruvu wilayani Bagamoyo. Akiwa kwenye mashamba ya kisasa ya korosho katika bonde hilo, Mkuu huyo wa mkoa amepata malalaniko mengi kutoka kwa wakulima ambao wameeleza kuwa wafugaji hao wanang’oa mazao yao na maeneo mengine walisha mifugo yao kwenye mazao ya chakula.

Wakati wa kuhutubia wakulima hao na wadau mbalimbali waliojumuika kusherehekea siku ya wakulima wa CHAURU maarufu kama CHAURU DAY, ametoa onyo kali kwa wafugaji popote pale walipo mkoani humo na kukemea tabia hiyo. “Tunawaheshimu sana wafugaji na tunawapenda. Tumewatengea zaidi ya ekari 40 elfu za malisho maeneo ya Ruvu (ilipokuwa ranchi ya taifa ya NARCO) na hivyo yeyote anaehitaji anakaribishwa. Lakini hatutakubali wala kumvumilia mfugaji yeyote atakaevunja sheria”, alisisitiza Mhandisi Ndikilo.

CHAURU DAY huazimishwa kila mwaka kusherehekea mafanikio na kuangazia changamoto mbalimbali ambazo wakulima wa umwagiliaji wa bonde hilo wanakumbana nazo. Mwaka huu CHAURU inaadhimisha mika 18 tangu kuanzishwa kwake.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akikagua shamba la nanasi lililopokatika eneo la chamba la CHAURU wakati wa kutembelea shamba hilo na kujionea shughuri zinazofanyika katika eneo hilo wakati wa kilele cha maadhimisho ya pili ya siku ya Chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu(CHAURU)
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo, viongozi wa CHAURU, pamoja na wadau wa kilimo wakishuhudia uvunaji wa mpunga katika moja ya shamba lililopo kwenye eneo la CHAURU wakati wa maadhimisho ya siku tatu ya Chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu(CHAURU).
Uvunaji wa mpunga ukiendelea
Baadhi ya mashamba ya mpunga yaliyopo katika eneo la CHAURU

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo  akiangalia maji yanaoingia kwenye mashamba ya wakulima wa CHAURU wakati wa maadhimisho ya siku tatu ya Chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu(CHAURU).
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akikagua baadhi ya bidhaa za Agricom Africa Ltd alipokuwa anatembelea mabanda ya wakulima pamoja na wadau wa kilimo wakati wa wakati wa kufunga maonesho ya siku tatu kuanzia  tarehe 08 hadi tarehe 10 Oktoba mwaka 2020 ikiwa ni maadhimisho ya miaka 18 ya kuanzishwa kwa Ushirika huo Chalinze mkoani Pwani.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akimsikiliza Mratibu wa usambazaji wa teknolojia na mahusiano TARI-Dakawa, Fabiola Langa apokuwa anatolea ufafanuzi kuhusu mbegu mbalimbali za mpunga zinazoweza kuinua kilimo na namna ya mkulima kuzitumia mbegu hizo wakati wa kufunga maonesho ya siku tatu kuanzia  tarehe 08 hadi tarehe 10 Oktoba mwaka 2020 ikiwa ni maadhimisho ya miaka 18 ya kuanzishwa kwa Ushirika huo Chalinze mkoani Pwani.
Meneja wa chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu(CHAURU) Victoria Olotu  akitolea ufafanuzi kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo kuhusu mchele  pamoja na Korosho zinazolimwa katika eneo hilo alipokuwa anatembelea baadhi ya mabanda mbalimbali kwenye maonesho yatakayofanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 08 hadi tarehe 10 Oktoba, 2020.
Mwenyekiti wa Bodi wa Chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu (CHAURU) Sadala Chacha kizungumza kuhusu historia ya ushirika huo ulioanzishwa mwaka 2002 pamoja na changamoto wanazozipata ndani na nje ya ushirika huo wakati wakati wa kufunga maadhimisho ya pili ya siku ya CHAURU yaliyoendana na maonesho ya Bidhaa za kilimo pamoja na mazao ya kilimo hicho kinachofanyika katika ushirika huo.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akitoa hotuba yake kwa viongozi na Wanachama wa chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu (CHAURU) waliofika kumsikiliza wakati wa kufunga maadhimisho ya pili ya siku ya CHAURU yaliyoendana na maonesho ya Bidhaa za kilimo pamoja na mazao ya kilimo hicho kinachofanyika katika ushirika huo.



Baadhi ya Wanachama wa chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu(CHAURU) pamoja na wananchi wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo wakati wa ufungaji wa wa maadhimisho ya pili ya siku ya CHAURU yaliyoanza taehe 08 hadi leo taehe Oktoba 10, 2010.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo  akitoa zawadi kwa wadau mbalimbali wa kilimo wa wakati wa ufungaji wa wa maadhimisho ya pili ya siku ya CHAURU yaliyoanza taehe 08 hadi leo taehe Oktoba 10, 2010.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo  tuzo ya shukrani kutoka kwauongozi wa chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu(CHAURU) wa wakati wa ufungaji wa maadhimisho ya pili ya siku ya CHAURU yaliyoanza taehe 08 hadi leo taehe Oktoba 10, 2010.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo  akionesha tuzo ya shukrani aliyopewa na uongozi wa CHAURU kwa kuweza kuwahamasiha kulia kilimo cha kisasa ili kufikia malengo waliyojiwekea kama ushirika wakati wa ufungaji wa wa maadhimisho ya pili ya siku ya CHAURU yaliyoanza taehe 08 hadi leo taehe Oktoba 10, 2010.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo  akipokea zawadi mbalimbali kutoka kwa wakulima wa chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu(CHAURU) wa wakati wa ufungaji wa maadhimisho ya pili ya siku ya CHAURU yaliyoanza taehe 08 hadi leo taehe Oktoba 10, 2020.


Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akiwa kwenye picha za pamoja na viongozi, wanachama na wadau wa kilimo wakati wa kufunga maadhimisho ya siku tatu ya Chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu(CHAURU).

No comments: