ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, October 15, 2020

“SHULE YA MSINGI SUNRISE YAFANYA MAHAFALI YA 13 TANGU KUANZISHWA KWAKE, WAZAZI WAPONGEZA”

Na Pius Ntiga, Dar es salaam

Afisa Elimu ya Msingi Wilaya ya Kinondoni Mkoa wa Dar es salaam, Kiduma Mageni, ameitaka Jamii kushirikiana na Walimu katika Malezi ya Wanafunzi lengo likiwa ni kukabiliana na vitendo vya Ukatili wa Kijinsia ikiwemo Ubakaji vinavyowakumba Wanafunzi.
Mageni ametoa kauli hiyo Mbezi Beach Jijini Dar es salaam wakati wa Mahafali ya 13 ya Darasa la Saba Shule ya Msingi ya Kimataifa Sunrise.

Katika Mahafali hayo Jamii imetakiwa kuacha Uonga ili kukwepa ushahidi na badala yake iwe msitari wa mbele kutoa taarifa pindi Mtoto anapofanyiwa vitendo vya Ukatili ambao kwa kiasi kikubwa humfanya akakosa ujasiri na badala yake kuwa na Ufaulu mdogo kutokana na kuumia Kisaikolojia.

“Niwambieni Wazazi na Walezi pamoja na Wanafunzi mnaonisikiliza hapa majuzi tu Ofisini kwangu nilikuwa nashughulikia kesi za Ubakaji ambayo Kimsingi inatokana na kutokuwa na Misingi mizuri ya Malezi yetu sisi Wazazi lakini kama tutawalea vizuri Wanafunzi hawa naamini matukio haya ya Ubakaji na Ukatili wa Kijinsia yataisha au kupungua kabisa.” Alisema Mageni.

Kwa mujibu wa takwimu za Wizaya ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto nchini mwaka 2017 pekee zaidi ya matukio 40,000 ya Ukatili wa Kijinsia yaliripotiwa.

Ili kutimiza Malengo ya Maendeleo Endelevu SDG’s husuani lengo namba tano la Usawa wa Kijinsia ifikapo 2030, Umoja wa Mataifa unaendelea kuzihimiza nchi Wanachama kuchukua hatua kuhakikisha Ukatili huo unakomeshwa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Shule ya Msingi Sunrise, Mama Mary Shirima, licha ya kujivunia ufundishaji mzuri katika Shule hiyo ambayo kati ya Shule Kumi za Manispaa ya Kinondoni zinazofundisha kwa Mchepuo wa Kiingereza, Shule hiyo imeshika nafasi ya Nane kwa ufaulu wa matokeo ya Elimu ya Msingi mwaka jana.

“Watoto wangu nawaomba sana msome zaidi kwa kweli maana Dunia ya sasa bila elimu mambo hayaendi, hivyo Elimu mliyoipata hapa iwe chachu ya mwanzo wenu wa mafanikio katika kujiunga na Kidato cha Nne mwakani.” Alisema Mama Shirima.

Nao baadhi ya Wazazi wanaosomesha Watoto wao katika Shule ya Sunrise wamepongeza juhudi mbalimbali zinazochukuliwa na uongozi wa Shule hiyo katika kukabiliana na matukio yakiwemo wa Utatili wa Kijisina na kusema juhudi hizo zikiwemo za ufundishaji ziendelee ili kuleta tija zaidi katika Shule hiyo ya Msingi Sunrise.

No comments: