Thursday, October 8, 2020

UMOJA NA MSHIKAMANO WAKIDUMISHA CHAMA CHA USHIRIKA WA WAKULIMA WA UMWAGILIAJI RUVU(CHAURU)

 

Afisa kilimo wa Chalinze Jovin Bararata akitoa hotuba yake kwa viongozi na Wanachama wa chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu(CHAURU) waliofika kumsikiliza wakati wa wa uzinduzi wa maadhimisho ya pili ya siku ya CHAURU yaliyoendana na maonesho ya Bidhaa za kilimo pamoja na mazao ya kilimo hicho kinachofanyika katika ushirika huo. Afisa huyo alimuwakilisha Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Chalinze.
Mwenyekiti wa Bodi wa Chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu(CHAURU) Sadala Chacha kizungumza kuhusu historia ya ushirika huo ulioanzishwa mwaka 2002 pamoja na changamoto wanazozipata ndani na nje ya ushirika huo wakati wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya pili ya siku ya CHAURU yaliyoendana na maonesho ya Bidhaa za kilimo pamoja na mazao ya kilimo hicho kinachofanyika katika ushirika huo.
Wanachama wa chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu(CHAURU) wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Afisa kilimo wa Chalinze Jovin Bararata aliyemwakilisha Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Chalinze katika uzinduzi wa maadhimisho ya pili ya siku ya CHAURU.
Afisa kilimo wa Chalinze Jovin Bararata akikata utepe kuashiria uzinduzi wa maadhimisho ya pili ya siku ya Chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu(CHAURU) itakayoedana na maonesho ya siku tatu kuanzia leo tarehe 08 hadi tarehe 10 Oktoba mwaka 2020.
Meneja wa NMB tawi la Mlandizi, Ephata Pallangyo  akiuzugumzia mikakati mbalimbali waliyoitumia kuwafikia Wanachama wa chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu(CHAURU) kwa kuweza kuwapa mikopo pamoja na kuwafungulia akaunti namba kwa ajili ya kujiwekea akiba pale wakulima hao wanapouza mazao wakati uzinduzi wa maadhimisho ya siku tatu Ushiika huo uliopo wilayani Chalinze mkoani Pwani.
Afisa Matekelezo Muandamizi wa NHIF Pwani, Ivo Edward Ndukeki akitoa maelezo kwa mgeni rasmi Afisa kilimo wa Chalinze Jovin Bararata kuhusu Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) unavyowafikia na kuwapa elimu kuhsu umuhimu wa kazi hizo Wanachama wa chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu(CHAURU) wakati uzinduzi wa maadhimisho ya siku tatu Ushiika huo uliopo wilayani Chalinze mkoani Pwani.
Afisa kilimo wa Chalinze Jovin Bararata (wa pili kulia) akishauliana jambo na Mwenyekiti wa Bodi wa Chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu(CHAURU) Sadala Chacha mara baada ya kupata maelezo kuhsu ufugaji wa samaki unaofanyika katika eneo la CHAULA wakati wa maadhimisho ya pili ya siku ya ushirika huo.
Afisa kilimo wa Chalinze Jovin Bararata akitoa maoni yake kwenye baadhi ya mbegu zakilimo zinazotumiwa na wakulima mbalimbali hasa wa ushirika wa CHAUMA wakati wa maonesho ya siku tatu kuanzia leo tarehe 08 hadi tarehe 10 Oktoba mwaka 2020 yaliyofanyika katika eneo la Ushirika huo Bagamoyo mkoani Pwani.
Afisa kilimo wa Chalinze Jovin Bararata akimsikiliza Mratibu wa usambazaji wa teknolojia na mahusiano TARI-Dakawa, Fabiola Langa apokuwa anatolea ufafanuzi kuhusu mbegu mbalimbali za mpunga zinazoweza kuinua kilimo na namna ya mkulima kuzitumia mbegu hizo wakati wa maonesho ya siku tatu kuanzia leo tarehe 08 hadi tarehe 10 Oktoba mwaka 2020 ikiwa ni maadhimisho ya miaka 18 ya kuanzishwa kwa Ushirika huo Chalinze mkoani Pwani.
Mgeni rasmi Afisa kilimo wa Chalinze Jovin Bararata  akiwa kwenye picha za pamoja na viongozi, wanachama na wadau wa kilimo mara baada ya kuzindua maadhimisho ya siku tatu ya Chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu(CHAURU).

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake