Thursday, October 8, 2020

Kwa Tabia Hizi, Utasubiri Sana Kuolewa!

RAFIKI, ni Ijumaa nyingine murua kabisa, karibu! Siku hizi wasichana wengi wazuri au warembo, ili kuwanasa, lazima uwahonge pesa nyingi!

Jamii imebadilika sana si kama zamani, ambapo mapenzi yalikuwa hayaangalii una pesa kiasi gani, mapenzi yalikuwa yanaangalia upendo wa dhati; yaani jinsi mtu anavyokupenda na malengo yake kwako.

Siku hizi msichana ukimhitaji kuwa naye kwenye uhusiano wa mapenzi, hata kama unaonana naye kwa mara ya kwanza barabarani, atakukubalia kwa maneno hapohapo na kukupa namba ya simu kama umemuomba.

Usidhani amekukubalia kwamba wewe ni mzuri sana au umemvutia kwa umbo au kwa maneno uliyompa, la hasha! Subiri dakika tu mkishapeana kisogo, halafu uangalie SMS zitakazoanza kuingia kutoka kwake.

Utakuta SMS kama baby naomba nisaidie pesa kidogo babu yangu anaumwa sana, nataka nikamuone kijijini. Tena anakuambia nitumie kwa simu, halafu maskini ya Mungu pengine babu yake anayesingizia anaumwa, alishafariki dunia miaka mingi iliyopita. Lengo ni kuanza kukulia pesa zako tu.

Ukishatuma hizo pesa za kwenda kumtazama babu yake, kesho utasikia naomba nitumie pesa kidogo nilikuwa ninadaiwa chuoni, sikumaliza ada!

Ukiona hivyo, ujue umeshakuwa mzazi wake. Rafiki nikuambie tu kwamba, kwenye mazingira kama haya, kuwa makini mno kwa sababu unaweza ukajikuta unapigwa pesa na kuambulia patupu!

Unachopaswa kujua ni kwamba, mwanamke huyo ataendelea hivyohivyo, akikuomba pesa ndogondogo hadi siku ya siku ambapo utashangaa imefika shilingi milioni moja, halafu ukimwambia mbona unazidi kuniomba pesa tu wakati sioni kama umenikubali kweli, utasikia atakachokwambia na utabaki umeduwaa.

yanayoendana na haya; “Vipesa vyako vinakuuma ehee! Kama vinakuuma nipotezee! Chukua time yako!”

Hapo hazungumzii kukurudishia pesa alizokula; yaani ameshakutenda, hapo utabaki unawaza bora hizo pesa ulizokuwa unamsaidia, ungefugia kuku wa nyama, pengine ungekuwa na biashara kubwa.

Ndivyo walivyo baadhi ya wanawake, hawana fadhila kwa wanaow-apenda kwa dhati.

Dada yangu, mwanaume akikupenda, anaweza akawa anakula mkate na maji analala ili tu apate pesa za kukupa zitakazo-kuwezesha kufanya unachotaka.

Mwanaume furaha yake, ni kukubaliwa na kupewa penzi, lakini mabinti wengi wakifanyiwa wema, huwa hawaku-mbuki mpaka siku wakishapewa mimba na kukataliwa, ndipo wanapochanganyikiwa wakidhani pesa nyingi ndiyo upendo mwingi.

Baadhi ya wanawake wa siku hizi, wakishamuona mwanaume ana kazi nzuri, wanadhani hapo ndipo pa kutegesha mimba ili waolewe, tena bila kufanya utafiti kama huyo anayemtegeshea mimba ana mke au hana mke.

Wanaume wengi wamedhulumiwa mno penzi na pesa zao zimeliwa. Wapo waliowasomesha mabinti tangu sekondari hadi chuo, kwa lengo la kuwaoa, lakini binti akishahitimu chuo na kupata kazi, anamsahau aliyemtoa mbali hadi akamfikisha hapo, anamwacha, tena na matusi juu. Sasa kama binti wewe hukumpenda mwanaume huyo, kwa nini ulipokea pesa zake kwa kudai na kumnunia wakati mwingine ili tu atoe pesa?

Mwanaume alikutegemea kukuoa asilimia zote, ndiyo maana akakusikiliza kwa kila shida uliyomwambia, leo unamuacha hivihivi ilhali akiwa amekug-haramia pesa nyingi sana. Uzuri wa msichana, unamfanya ahitajiwe kila siku na watu tofautitofauti.

Kwa hiyo wewe kijana wa kiume, ukishaanza uhusiano na msichana huyu mzuri, lazima atakufanya umsikilize kwa kila kitu atakach-okisema na ukikosea kidogo tu, mfano amekuomba shilingi elfu hamsini ya kwenda kusuka nywele, bahati mbaya siku hiyo ukawa huna na ukamwambia ukweli kuwa leo sina, basi hapohapo atachukulia ndiyo sababu na kuanza kukutumia ujumbe mfupi wa dharau na kukuambia; “Nipotezee, kama hutaki kunipa hiyo pesa, basi kaa nayo!”

Japo anajua ametumia pesa zako nyingi, lakini anatuma ujumbe wa kuonesha hakutaki tena, eti humjali, sasa unabaki unajiuliza kama ungekuwa humjali ungemgharamia pesa zote ulizompa awali?

Hutapata jibu na utabaki unalalamika moyoni, kuwa bora usingempa hata shilingi moja na pesa hizo, bora ungewasaidia maskini ili Mungu akupe thawabu. Wasichana kama hawa, tunawapa sifa ya ziada kuwa wana roho mbaya na ndiyo maana Mungu anawapa adhabu ya kutoolewa na kulea watoto peke yao kwa taabu maishani mwao.

Itaendelea wiki ijayo.
Mahaba Xclusive
Hashim Aziz
+255 719401968

1 comment:

  1. Thanks for sharing this! I’m delighted with this information, where such important moments are captured. All the best!

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake