WATU watatu wamefariki dunia kufuatia shambulio lililotokea katika Mji wa Nice nchini Ufaransa kanisani kwenye ibada ya asubuhi ambalo Rais Emmanuel Macron ameliita ni shambulio la kigaidi akihusisha makundi ya Kiislam yenye misimamo mkali.
Kwa mujibu wa polisi mtuhumiwa ambaye ni mawanaume 21, raia wa Tunisia, yupo chini ya ulinzi akiendelea kupatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa na risasi za polisi.
Ufaransa imeongeza tahadhari yake ya usalama wa kitaifa kufikia kiwango cha juu na wanajeshi zaidi ya 4,000 wanapelekwa kulinda makanisa na shule katika miji mikubwa.
Chanzo cha shambulio hilo hakijafahamika, lakini linakuja siku chache baada ya Macron kutetea uchapishaji wa katuni zinazomuonyesha Mtume Mohammad.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake