Wednesday, November 18, 2020

NAIBU KATIBU VIWANDA NA BIASHARA AFANYA ZIARA KATIKA VIWANDA VYA SARUJI NA MAWAKALA WAKE KUFANYA TATHIMINI YA UPANDAJI WA BEI NA UPATIKANAJI WAKE

Naibu katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Bw.Ludovick J.Nduhiye akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Portland Cement Tanzania Bw. Alfonso Velez kuhusu Changamoto ya upandaji bei cement na jinsi Kampuni hiyo inayozalisha cement ya Twiga. Mazungumzo hayoyalifanyika katika ofisi za kampuni hiyo , Wazo Jijini Dar es salaam tarehe 16/11/2020 ikiwa ni muendelezo wa ziara ya kutembelea Viwanda na wasambazaji wa Cement ili kufanya tathimini ya changamoto hiyo na jinsi ya kukabiliana nayo.
Naibu katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Bw.Ludovick J.Nduhiye akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Portland Cement Tanzania Bw. Alfonso Velez kuhusu Changamoto ya upandaji bei cement na jinsi Kampuni hiyo inayozalisha cement ya Twiga ilivyojipanga kupunguza usafirishaji wa cement nje ya nchi ili kukabiliana na changamoto iliyopo. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi za kampuni hiyo , Wazo Jijini Dar es salaam tarehe 16/11/2020 ikiwa ni muendelezo wa ziara ya kutembelea Viwanda na wasambazaji wa Cement ili kufanya tathimini ya changamoto hiyo na jinsi ya kukabiliana nayo
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Portland Cement Tanzania (TPCCL) Alfonso Velez akitoa maelezo kwa Naibu katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Ludovick J. Nduhiye kuhusu jinsi Kampuni hiyo inayozalisha cement ya Twiga ilivyojipanga kukabiliana na changamoto hiyo , Wapili kushoto ni Bw. Richard Magoda meneja wa Mazingira wa TPCCL na wa pili kulia ni Bw. Christopher Nassari Kaimu Mkurugenzi Idara ya Biashara Wizara ya Viwanda na Biashara . Mazungumzo hayoyalifanyika katika ofisi za kampuni hiyo, Wazo Jijini Dar es salaam tarehe 16/11/2020 ikiwa ni muendelezo wa ziara ya kutembelea Viwanda na wasambazaji wa Cement ili kufanya tathimini ya changamoto hiyo na jinsi ya kukabiliana nayo.
Naibu katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Ludovick J. Nduhiye akizungumza na Katibu Tawala wa Mkoa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Bw. Paulo Mshimo Makanza Ofisini kwake Jijini Dar es salaam tarehe 16/11/2020 kuhusu changamoto ya upandaji bei cement na jinsi ya kukabiliana nayo. Huu ni muendelezo wa ziara inayofanywa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda katika kufanya tathimini ya Uapandaji bei Cement na Vifaa vya ujenzi.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake