Saturday, December 19, 2020

WATOTO 600,KUNUFAIKA NA ELIMU, LONGIDO.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la World Vision Kanda ya Kaskazini bw.Mkama Nangu akifundisha Watoto ambao hawapo pichani wakati wa makabidhiano ya madarasa.
Wanafunzi wakiwa katika madarasa mapya yaliyojengwa na Shirika hilo,ambao wanapata Elimu katika shule ya msingi Noondoto ambao baada ya kufunguliwa watapata Elimu katika shule ya msingi Engusero.
Mkuu wa Wilaya ya Longido Frank Mwaisumbe akipokea maelezo ya mradi huo kutoka kwa katibu tarafa ya Ketumbeine Pamoja na mratibu wa Mradi wa World Vision Ketumbeine AP.

Na.Mwandishi wetu – Longido

Shirika lisilo la kiserikali la World Vision limekabidhi madarasa mawili na Ofisi ya walimu ya shule ya msingi Engusero,vilivyogharimu kiasi cha shilingi 73,512,000,kwa Mkuu wa wilaya ya longido Frank Mwaisumbe.

Akikabidhi mradi huo uliojengwa kwa ufadhili wa Shirika la World Vision Ketumbeine AP, Mkurugenzi mkuu wa Shirika hilo Kanda ya Kaskazini,Bw.Mkama Nangu alisema kuwa ujenzi wa shule hiyo ulianza March 2020,baada ili kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano na wananchi wa Engusero,ambao walishaanza ujenzi wa madarasa mengine.

Alisema kuwa kukamilika kwa shule ya msingi Engusero kutanufaisha zaidi ya watoto 600,ambao walikuwa wanapata elimu ya msingi katika shule ya msingi Noondoto,ambao pia walikuwa wanatembea umbali mrefu kutafuta elimu.

Bw.Mkama alisema kuwa kutokana pia na juhudi za wananchi ambazo walionyesha kwa kuanza ujenzi wa madarasa matatu kwa nguvu zao ambayo,yamefika hatua ya boma(lenta) ili kunusuru maendeleo hafifu ya kielimu kwa watoto wao ambao mbali na kutembea umbali mrefu lakini pia huatarisha maisha kwa kuwa wilaya hiyo imezungukwa na wanyama.

“Shirika la World Vision Ketumbeine AP ambalo ndio mfadhili mkuu katika shule yetu hii liliamua kuunga juhudi za wananchi wa Kijiji cha Engusero na Serikali yetu chini ya raisi dkt.John Pombe Magufuli kwa kujenga madarasa mawili na Ofisi ya walimu,ambayo Sasa yamekamilika na yapo tayari kutumika ili kuhakikisha kuwa kuna ustawi wa mtoto,ndani ya eneo letu kwa Maisha ya sasa na baadae”.Alisema Mkama.

Nae Mkuu wa Wilaya hiyo Frank Mwaisumbe amelipongeza Shirika hilo kwa kuamua kuwezesha ujenzi wa shule hiyo pamoja kuahidi kuwa serikali imeyapokea majengo hayo na itayatunza ili kufanya kazi husika.

“Wananchi wa Engusero katika kata hii ya Noondoto nimeambiwa kuwa mmejenga madarasa haya matatu hivyo Serikali itayamalizia kwa maana ya kutambua mchango wa nguvu zenu,pia mmejenga vyoo bora vya matundu 8,pia ni hatua kubwa saana hii kwetu na eneo hili Sasa watoto watasoma hapa na kuepuka,kutembea umbali mrefu na uchovu ambao huzorotesha maendeleo ya mtoto kielimu.”Alisema Mwaisumbe.

Aidha ameiagiza Halmashauri ya wilaya hiyo chini ya Mkurugenzi wake bw. Dkt.Jumaa Mhina kuhakikisha kuwa shule hiyo inasajili na kukamilika kabla ya February 2021,lakini pia inamalizia madarasa matatu ili watoto waanze kusoma Mara moja.

“Nitamke kuwa mpaka tarehe 30 February 2021,shule hii iwe imekamilika na nikute watoto hapa,madarasa ya awali wote mtoto kutembea kilomita 20 hadi 19,ni mbali sana na mkumbuka wilaya yetu ina wanyama wakali tunusuru Maisha ya watoto hawa,na fidia za umeme nataka zitumike hapa na nitakuja mwenyewe na sintataka kisingizio.”alisema Mwaisumbe

Hata hivyo wananchi hao wameweza kutumia nguvu zao kuweza kutumia kiasi cha shilingi Milioni 23,000,000, kujenga madarasa mengine matatu ambayo yamefika hatua ya lenta,pamoja na kujenga choo chenye matundu 8,kwa gharama ya shilingi Milioni 17,000,000.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake