Saturday, December 19, 2020

WAZIRI MWAMBE ATAKA MAGEUZI MAKUBWA KATIKA SEKTA VIWANDA NA BIASHARA HAPA NCHINI.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mheshimiwa Geoffrey Mwambe akizungumza wakati akifungua Balaza la wafanyakazi wa Wizara ya Viwanda na Biashara walipokutana kutathmini mipango waliyojiwekea na kuweka mipango mipya mkutano umefanyika jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Profesa Riziki Shemdoe akizungumza wakati wa ufunguzi wa balaza la wafanyakazi wa Wizara ya Viwanda na Biashara walipokutana kutathmini mipango waliyojiwekea na kuweka mipango mipya mkutano uliofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa utawala na rasilimali watu wizara ya Viwanda na Biashara Bwana Issa Ng’imba akizungumza wakati wa ufunguzi wa balaza la wafanyakazi wa Wizara ya Viwanda na Biashara walipokutana kutathmini mipango waliyojiwekea na kuweka mipango mipya mkutano uliofanyika jijini Dodoma. Waziri wa Viwanda na Biashara Mheshimiwa Geoffrey Mwambe, wanne kutoka kulia mstari wa mbele akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa balaza la wafanyakazi la wizara hiyo mara baada ya ufunguzi wa balaza hilo lililofanyika jijini Dodoma kwa lengo la kutathmini mikakati waliyojiwekea na kuweka mikakati mipya.

Na Ezekiel Mtonyole – Dodoma.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Geoffrey Mwambe amewataka watendaji katika Wizara hiyo kufanya kazi kwa weredi na ubunifu mkubwa ili kuleta mageuzi makubwa katika Wizara hiyo na kuongeza uwezo wa kuibua wawekezaji wapya wazawa hapa nchini.

Waziri Mwambe ametoa wito huo jijini Dodoma wakati akifungua mkutano wa balaza la wafanyakazi wa Wizara hiyo, ambapo amesema kila mtendaji na wakuu wa idara mbalimbali katika Wizara kuhakikisha wanafanyakazi kwa bidii na kuibua wawekezaji wapya hapa nchini.

“Kila mtumishi katika kitengo chake au idara wafanyekazi kwa weredi mkubwa natamani mabadiliko makubwa na kwa mda mfupi kila mtendaji ajitambue na ujitafakari utalifanyia nini taifa lako” amesema.

Amesema nchi inafulsa nyingi sana ambazo zingeweza kuwanufaisha watanzania lakini walioaminiwa kusimamia vitengo hivyo bado hawajafanya kitu cha ajabu ambacho kitawanufaisha watanzania kuinua sekta hiyo.

Waziri Mwambe amesema Wizara ndio wahamasishaji na wawezeshaji wa shughuli za viwanda hapa nchini hivyo wanatakiwa kujitoa kwa nguvu zao zote na akili zao zote kuhakikisha sekta hiyo inakua hapa nchini na kuwanufaisha watanzania.

Ametaka kuboreshwa kwa kitengo cha huduma kwa wateja katika Wizara ili kuwakaribisha wawekezaji na sio kutoa kauli mbaya kwa wateja wanaohitaji huduma katika Wizara hiyo ambayo inaweza kunufaisha wananchi endapo wananchi watahamasika kuanzisha biashara.

Amewataka watendaji na wasimamizi katika wizara kujenga utaratibu wa kuwapa motisha wafanyakazi wanaofanyakazi kwa waminifu ili kuwaongezea motisha kwamba jitihada hizo zitahamasisha utandaji kazi katika Wizara, sambamba na kusimamia ushirikishwaji kwa watumishi wote katika majukumu na sio kubagua.

“Katika hili hakikisheni ushirikishwaji kwa watumishi na kugawa majumu sawa kwa watumishi wote na kutowabagua kitendo cha kuwabagua au kutoa majukumu kwa upendeleo itashusha morali kwa watumishi” amesema.

Pia amehamasisha wakuu wa idara kutoa nafasi kwa watumishi wao kujiendeleza kimasomo na hiyo inasaidia katika kuimarisha watumishi kuwapanua kimawazo watumishi hao na kuwapandisha katika nafasi zao, sambamba na kuwaonyesha nafasi za juu.

“Nina ushahidi wapo walioanza kazi kama masekretari katika ofisi lakini wakajiendeleza na hatimaye wakaja wakawa wakuu wa idara, kwahiyo unaweza ukaanza kama dereva lakini ukamaliza kama Katibu mkuu hiyo ni heshima kubwa sana” amesema.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Profesa Rikizi Shemdoe amesema mkutano huo ni wa pili tangu kuzinduliwa kwa Balaza hilo na katika mkutano huo watatumia kutathmini waliyokubaliana katika mkutano wa kwanza na kuweka mikakati mipya ya kutekeleza kwa mwaka huu.

Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wajumbe wengine Mkurugenzi wa utawala na rasilimali watu wizara ya Viwanda na Biashara Bwana Issa Ng’imba amesema kwa kushirikiana na wenzake watahakikisha wanayafanyia kazi maagizo yote yaliyotolewa na kufanyakazi kwa weredi

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake