Saturday, January 2, 2021

Membe Abwaga Manyaga ACT-Wazalendo


ALIYEKUWA mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha ACT-Wazalendo na mshauri wa chama hicho, Bernard Membe, ametangaza rasmi jana Desemba Mosi kujiuzulu nafasi zake zote ndani ya chama hicho.

Hatua ya kujiuzulu ameitangaza akiwa nyumbani kwake katika Kijiji cha Rondo- Chiponda, Wilaya ya Mtama Mkoa wa Lindi nchini Tanzania jana Ijumaa tarehe 01 Januari 2021, wakati akizungumza na DW na kueeleza kuwa hajafanya uamuzi huo kwa shinikizo lolote na kwamba kwa sasa atakuwa mshauri wa masuala mbalimbali yanayoihusu nchi ya Tanzania na kupigania demokrasia ya kweli.

Hata hivyo, hakutoa ufafanuzi zaidi juu ya sababu ya kuchukua maamuzi hayo. Membe amesema,tayari ameandika barua ya kujiuzulu kwa kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe kama utaratibu unavyotaka.

Hata hivyo, waziri huyo wa zamani wa mambo ya nje wa Tanzania katika utawala wa awamu ya nne ya Jakaya Mrisho Kikwete amesema, kwa sasa ni mapema kubainisha mwelekeo wake unaofuata katika vyama vya siasa.

Membe aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania kati ya 2007 hadi 2015 ametangaza uamuzi huo leo akiwa nyumbani kwake kijijini Rondo Chiponda, Wilaya ya Mtama Mkoani Lindi ambapo amesema hajafanya uamuzi huo kwa shinikizo lolote na kwamba kwa sasa atakuwa mshauri wa masuala mbalimbali yanayoihusu nchi ya Tanzania na kupigania demokrasia ya kweli.

Mwanadiplomasia huyo alitangaza kuhamia Chama cha ACT Wazalendo miezi michache kabla ya uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2020 baada ya kufukuzwa uanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) tarehe 28 Februari 2020 na Kamati Kuu ya chama hicho, kisha uamuzi huo kubarikiwa na Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), tarehe 10 Julai 2020.

Membe alifukuzwa kwa tuhuma za ukiukwaji wa maadili ya CCM, pamoja na kuonywa mara kadhaa, pasina kubadilika. Baada ya kuhamia ACT Wazalengo, Membe alitangaza kugombea kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho 

GPL

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake