Saturday, January 2, 2021

RAIS WA ZANZIBAR DK HUSSEIN ALI MWINYI AMEMUAPISHA KATIBU WA BARAZA LA MAPINDUZI NA KATIBU MKUU KIONGOZI LEO IKULU

WAKUU wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Zanzibar wakifuatilia hafla ya kuapishwa kwa Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said, wakati wa hafla hiyo iliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo.(Picha na Ikulu)
BAADHI ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakifuatilia kuapishwa kwa Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said, wakati wa hafla hiyo iliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mhandisi Zena Ahmed Said kua Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, hafla hiyo ya kuapishwa imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar, 2/1/2021.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi Hati yake ya Kiapo Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said, baada ya kuisain, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
MTEULE Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said, akiwa katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar akisubiri kuapishwa kuwa Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) hafla hiyo imefanyika leo 2/1/2021 Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisaini Hati ya Kiapo ya Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said, baada ya kumuapisha katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
KATIBU wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mstaaf Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee na (kushoto kwake) Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Dkt. Mwinyi Talib Haji, Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi, Askofu wa Jimbo la Zanzibar Kanisa la TAG. Rev.Dikson Kaganga na Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Hassan Othman Ngwali, wakifuatilia hafla ya kuapishwa kwa Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said, hafla hiyo iliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo.(Picha na Ikulu)KATIBU wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said akiwa katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar baada ya kuapishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) na (kulia kwake) Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid na (kushoto kwake) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mstaaf Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Dkt. Mwinyi Talib Haji, wakiwa katika ukumbi wa Ikulu wakati wa hafla hiyo.(Picha na Ikulu)

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake