Chanzo chetu cha karibu kabisa na mrembo huyo, kimesema kuwa, Sarah aliamua kurudi kwao kwa sababu ya kuchoka na vituko vya Harmo tangu ilipojulikana kuwa ana mtoto wa nje na kuamua kumuweka hadharani.
“Unajua Sarah aliamua kunyoosha mkono juu na kusepa zake nchini kwao maana alishindwa kuvumilia kila kukicha visa hivyo aliona wazi hapendwi wala hathaminiwi,” alisema mtoa habari huyo.
Akiendelea kushusha ubuyu kama wote, mtoa habari huyo alisema, Sarah aliamua kuondoka kwa ajili ya kutotaka kukumbuka chochote walichokuwa wakishea na msanii huyo akiwa hapa nchini na kubadilisha mazingira mengine kabisa ili kupunguza machungu aliyokuwa nayo.
“Sarah ameondoka kwao lakini alikuwa na maumivu makali sana akaona bora aondoke labda anaweza kupunguza machungu aliyokuwepo nayo kutokana na Harmonize kumsaliti na kubadilisha kabisa hali ya hewa,” alisema mtu huyo ambaye ni wa karibu na Sarah.
Gazeti hili lilijaribu kumtafuta kwa njia ya meseji ya moja kwa moja kupitia mtandao wake wa Instagram lakini hata hivyo hakutoa ushirikiano wowote.
Sarah na Harmo walioishi kwa miaka kadhaa bila kupata mtoto, walifunga ndoa ya kimila nchini Italy na kufanya tafrija nyingine hapa Bongo kabla ya kumwagana na kila mtu kushika hamsini zake.Kwa sasa Harmo ameonesha kujitosa mzimamzima kwenye penzi la mrembo kutoka Bongo Movies, Kajala Masanja
chanzo GPL
No comments:
Post a Comment