ANGALIA LIVE NEWS

Friday, February 12, 2021

SERIKALI: TANZANIA HAIJAWAHI KUSEMA HAINA VIRUSI VYA CORONA

MSEMAJI wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas, amesema Tanzania haijawahi kusema haina virusi vya corona na kwamba Tanzania ni sehemu ya dunia ambapo kuna raia wa kigeni wanaokuja nchini na wapo Watanzania wanaokwenda nje, hivyo muingiliano upo.

Katika mahojiano na BBC Swahili, ameeleza serikali inachosema ni Tanzania imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kudhibiti maambukizi ya #COVID19 kwa njia za kisayansi na za asili. Pia, serikali ilikuwa makini tangu mapema.

Aidha, amesema Tanzania haijadharau chanjo za corona na kufafanua kuwa chanjo nyingi zipo katika majaribio, hivyo ni vyema zikaendelea kufanyiwa majaribio ili usahihi wake wa kisayansi uweze kuthibitika.

Amesema: “Dunia nzima kuna kelele, yapo maeneo hizo chanjo zimeleta athari kubwa kwenye afya ya binadamu. Sisi kama nchi hatuwezi kuwa sehemu ya majaribio.

No comments: