ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, February 16, 2021

WAITARA ATOA AGIZO KWA NEMC KUFANYA UTAFITI KINA CHA MAJI YA MAZIWA MKOANI SINGIDA

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mwita Waitara akizungumza na viongozi mbalimbali kutoka Wilaya ya Singida mara baada ya kuwasili mkoani Singida kwa ziara ya kikazi kwa lengo la kuhimiza uzingatiaji wa Sheria ya Mazingra ya mwaka 2004 na kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira hususan upandaji na utunzaji wa miti kwa kila halmashauri.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mwita Waitara akipokea taarifa za mazingira za halmashauri za Singida mara baada ya kuwasili Ofisi ya Mkuu wa wilaya Singida kwa ziara ya kikazi kwa lengo la kuhimiza uzingatiaji wa Sheria ya Mazingra ya mwaka 2004 na kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira hususan upandaji na utunzaji wa miti kwa kila halmashauri.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mwita Waitara (kushoto) akifurahia jambo na viongozi mbalimbali kutoka Wilaya ya Singida mara baada ya kuwasili mkoani Singida kwa ziara ya kikazi kwa lengo la kuhimiza uzingatiaji wa Sheria ya Mazingra ya mwaka 2004 na kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira hususan upandaji na utunzaji wa miti kwa kila halmashauri.
Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhe. Paskasi Muragiri akitoa neno la ukaribisho kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mwita Waitara aliyewasili ofisini kwake kwa ajili ya kufanya ziara ya kikazi wilayani humo kwa lengo la kuhimiza uzingatiaji wa Sheria ya Mazingra ya mwaka 2004 na kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira hususan upandaji na utunzaji wa miti kwa kila halmashauri.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mwita Waitara (katikati) akiwa katika kikao na maafisa mazingira (hawapo pichani) kutoka Wilaya na Manispaa ya Singida kwa lengo la kuwapa maelekezo mbalimbali. Wengine kuanzia kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida Mhe. Elia Digha, Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhe. Paskasi Muragiri Meya wa Manispaa ya Singida Mhe. Yagi Maulidi Kiaratu na Katibu Tawala Wilaya ya Singida Hassan Ngoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mwita Waitara (kushoto) akitoa maelekezo alipotembelea dampo la Manispaa ya Singida alipofanya ziara ya kikazi kwa lengo la kuhimiza uzingatiaji wa Sheria ya Mazingra ya mwaka 2004 na kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira hususan upandaji na utunzaji wa miti kwa kila halmashauri.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mwita Waitara akizungumza na wafanyabiashara na wananchi alipotembelea soko katika Manispaa ya Singida kukagua miundombinu ya kukusanya na kuhifadhi taka ngumu wakati alipofanya ziara ya kikazi kwa lengo la kuhimiza uzingatiaji wa Sheria ya Mazingra ya mwaka 2004 na kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira hususan upandaji na utunzaji wa miti kwa kila halmashauri.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mwita Waitara (wa pili kushoto) akisikiliza maelezo kuhusu mradi wa machinjio ya Manispaa ya Singida alipofanya ziara ya kikazi kwa lengo la kuhimiza uzingatiaji wa Sheria ya Mazingra ya mwaka 2004 na kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira hususan upandaji na utunzaji wa miti kwa kila halmashauri.
(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)

Naibu‌ ‌Waziri‌ ‌Ofisi‌ ‌ya‌ ‌Makamu‌ ‌wa‌ ‌Rais‌ ‌(Muungano‌ ‌na‌ ‌Mazingira)‌ ‌Mhe.‌ ‌Mwita‌ ‌ Waitara‌ ‌ameliagiza‌ ‌Baraza‌ ‌la‌ ‌Taifa‌ ‌la‌ ‌Hifadhi‌ ‌na‌ ‌Usimamzi‌ ‌wa‌ ‌Mazingira‌ ‌(NEMC)‌ ‌kufanya‌ ‌utafiti‌ ‌kuangalia‌ ‌namna‌ ‌ya‌ ‌kudhibiti‌ ‌kuongezeka‌ ‌kwa‌ ‌kina‌ ‌cha‌ ‌ maji‌ ‌ya‌ ‌maziwa‌ ‌mkoani‌ ‌Singida.‌ ‌

Ameliagiza‌ ‌Baraza‌ ‌hilo‌ ‌kufanya‌ ‌tathmini‌ ‌na‌ ‌kutoa‌ ‌suluhisho‌ ‌la‌ ‌kuongezeka‌ ‌kwa‌ ‌kina‌ ‌cha‌ ‌maji‌ ‌katika‌ ‌Ziwa‌ ‌Masogweda‌ ‌na‌ ‌Mulya‌ ‌katika‌ ‌manispaa‌ ‌na‌ ‌wilaya‌ ‌ya‌ ‌Singida‌ ‌ambayo‌ ‌yamefurika‌ ‌na‌ ‌kuleta‌ ‌madhara‌ ‌katika‌ ‌makazi‌ ‌na‌ ‌mashamba.‌ ‌

Waitara‌ ‌alitoa‌ ‌agizo‌ ‌hilo‌ ‌jana‌ ‌wakati‌ ‌wa‌ ‌ziara‌ ‌ya‌ ‌kikazi‌ ‌mkoani‌ ‌humo‌ ‌baada‌ ‌ya‌ ‌kupata‌ ‌maelezo‌ ‌kutoka‌ ‌kwa‌ ‌Mkuu‌ ‌wa‌ ‌Wilaya‌ ‌ya‌ ‌Singida‌ ‌Mhe.‌ ‌Paskasi Muragiri‌ ‌ambaye‌ ‌aliomba‌ ‌zichukuliwe‌ ‌hatua‌ ‌kukabiliana‌ ‌na‌ ‌hali‌ ‌hiyo.‌ 

Muragiri alisema‌ ‌ziwa‌ ‌hilo‌ ‌huenda‌ ‌likazingira vijiji‌ ‌hivyo viwili‌ ‌na‌ ‌kusababisha‌ ‌madhara‌ ‌kwa‌ ‌wakazi‌ ‌wanaoishi‌ ‌humo‌ ‌hivyo‌ ‌alitumia‌ ‌nafasi‌ ‌hiyo‌ ‌kumuomba‌ ‌Naibu Naibu‌ ‌Waziri‌ ‌huyo‌ ‌kulifanyia‌ ‌kazi‌ ‌suala‌ ‌hiyo‌ ‌katika‌ ‌ngazi‌ ‌ya‌ ‌kitaifa.‌ ‌

Katika‌ ‌ziara‌ ‌hiyo‌ ‌pamoja‌ ‌na‌ ‌mambo‌ ‌mengine‌ ‌Waitara‌ ‌alitembelea‌ ‌machinjio‌ ‌katika‌ ‌manispaa‌ ‌hiyo‌ ‌na‌ ‌kuitaka‌ ‌halmashauri‌ ‌hiyo‌ ‌kuharakisha‌ ‌mpango‌ ‌wa‌ ‌kuihamishia‌ ‌eneo‌ ‌lingine‌ ‌walilotenga.‌“Niwapongeze‌ ‌viongozi‌ ‌wa‌ ‌manispaa‌ ‌ya‌ ‌Singida‌ ‌nimesikia‌ ‌hapa‌ ‌mna‌ ‌mpango‌ ‌wa‌ ‌kujenga‌ ‌machinjo‌ ‌nyingine‌ ‌kwani‌ ‌baada‌ ‌ya‌ ‌hii‌ ‌na‌ ‌nina‌ ‌imani‌ ‌itakuwa‌ ‌ya‌ ‌kisasa‌ ‌na‌ ‌itakidhi‌ ‌mahitaji‌ ‌maana‌ ‌sasa‌ ‌hivi‌ ‌ninyi‌ ‌ni‌ ‌manispaa‌ ‌na‌ ‌mnahitaji‌ ‌eneo‌ ‌kubwa‌ ‌kuliko‌ ‌hili,”‌ ‌alisema.‌ ‌

Pia‌ ‌katika‌ ‌ziara‌ ‌hiyo‌ ‌alitembelea‌ ‌soko‌ ‌kuu‌ ‌na‌ ‌kuridhishwa‌ ‌na‌ ‌hali‌ ‌ya‌ ‌miundombinu‌ ‌ya‌ ‌kuhifadhi‌ ‌taka‌ ‌ngumu‌ ‌pamoja‌ ‌na‌ ‌dampo‌ ‌lililopo‌ ‌katika‌ ‌eneo‌ ‌la‌ ‌Manga‌ ‌nje‌ ‌kidogo‌ ‌ya‌ ‌manispaa‌ ‌hiyo.‌ ‌

Akizungumza‌ ‌katika‌ ‌kikao‌ ‌na‌ ‌maafisa‌ ‌mazingira‌ ‌kutoka‌ ‌manispaa‌ ‌hiyo‌ ‌Waitara‌ ‌alisema‌ ‌ipo‌ ‌haya‌ ‌ya‌ ‌kuwashirikisha‌ ‌wananchi‌ ‌katika‌ ‌maeneo‌ ‌yao‌ ‌katika‌ ‌masuala‌ ‌ya‌ ‌kuhifadhi‌ ‌mazingira‌ ‌ili‌ ‌kupata‌ ‌taarifa‌ ‌kutoka‌ ‌kwenye‌ ‌vijiji‌ ‌ngazi‌ ‌ya‌ ‌chini.‌ ‌Naibu‌ ‌Waziri‌ ‌Waitara‌ ‌yuko‌ ‌katika‌ ‌ziara‌ ‌mikoa‌ ‌mbalimbali‌ ‌kwa‌ ‌lengo‌ ‌la‌ ‌kuhimiza‌ ‌uzingatiaji‌ ‌wa‌ ‌Sheria‌ ‌ya‌ ‌Mazingra‌ ‌ya‌ ‌mwaka‌ ‌2004‌ ‌na‌ ‌kutoa‌ ‌elimu‌ ‌ya‌ ‌utunzaji‌ ‌wa‌ ‌mazingira‌ ‌hususan‌ ‌upandaji‌ ‌na‌ ‌utunzaji‌ ‌wa‌ ‌miti‌ ‌kwa‌ ‌kila‌ ‌halmashauri.‌

No comments: