Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa baada ya kipindi cha kutambulisha wageni waliotembelea Bunge leo Jumatatu Mei 10 2021.
Amesema baada ya kuahirishwa wa mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga ulitakiwa kuchezwa Mei 8 mwaka huu na kulisababisha mijadala katika mitandao ya jamii lakini pia kutojua kwa hatima ya waliolipa kiingilio katika mchezo huo.
Amesema tukio hilo limevuta hisia Kwa Watanzania ndani na nje kwasababu timu hizi ndizo zimebeba taswira ya mpira wa miguu Tanzania.
“Kufuatia kero tayari tumeagiza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuhakikisha wanatoa taarifa haraka sana kwa Watanzania mchezo wenyewe utachezwa lini lakini kuna viingilio ambavyo walikuwa wametoa hatma yake nini,”amesema.
Amesema wizara hiyo inatakiwa kutoa taarifa hiyo kwa kushirikiana na chombo kinachosimamia mchezo huo cha Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF).ADVERTISEMENT
“Naomba kuwasihi watanzania hasa wapenzi wa michezo kwenye eneo la mpira wa miguu ambao walijiandaa kusikia na kuangalia mpira wa miguu tuipe muda wizara itoe taarifa kwa kushirikiana na taasisi inayoshughulikia mpira wa miguu TFF wapate kujua hatma,” amesema Majaliwa.
Mwanaspoti
No comments:
Post a Comment