ANGALIA LIVE NEWS

Monday, May 10, 2021

WAZIRI MKENDA AWAITA WAWEKEZAJI KUWEKEZA KATIKA SEKTA YA HOTELI JIJINI DODOMA

Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda akifungua kitambaa kuashiria uzinduzi rasmi wa Hoteli ya Rafiki Dodoma Hotel Jijini Dodoma Mei 8, 2021. Hoteli hiyo imejengwa na muwekezaji mzawa Bw. Fladimiry Mallya kutoka Rombo mkoani Kilimanjaro.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini Mhe. Antony Mavunde akikata utepe kuzindua Hoteli ya Rafiki Dodoma Hotel Mei 8, 2021.
Muonekano wa Hoteli ya Rafiki Dodoma Hotel baaada ya kuzinduliwa na Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda Mei 8, 2021 Jijini Dodoma.
Mmiliki wa Hoteli ya Rafiki Dodoma Hotel iliyozinduliwa Jijini Dodoma Mei 8, 2021 Bw. Fladimiry Mallya kutoka Rombo mkoani Kilimanjaro akifurahia jambo na Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini Mhe. Antony Mavunde mara baada ya Hoteli hiyo kuzinduliwa na Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda
Mshauri wa Hoteli ya Rafiki Dodoma Hoteli Bw. Barrik Daniel (kushoto) akitoa maelezo kwa Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda (Mb) kuhusu huduma zinazotolewa katika Hoteli hiyo kabla kuizindua Mei 8, 2021.

Na.Alex Sonna, Dodoma

SERIKALI amewaasa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuja kuwekeza katika sekta ya Hoteli Jijini Dodoma kutokana na fursa zilizopo zinazoendana na kukua kwa Jiji hilo.

Ameyasema hayo Mei 8, 2021 na Waziri wa Kilimo Mhe. Prof. Adolf Mkenda,wakati akizundua hoteli ya Rafiki Dodoma Hotel yenye hadhi ya nyota nne iliyojengwa na muwekezaji mzawa Bw. Fladmiry Mallya kutoka Rombo mkoani Kilimanjaro.

Waziri Mkenda amesema kuwa wawekezaji wanahitaji katika jiji la Dodoma kutokana na uwepo wa shughuli nyingi za kiserikali na kitaifa ambazo zinahitaji uwekezaji katika huduma mbalimbali.

Akizungumzia uzinduzi wa Hoteli hiyo Prof. Mkenda amesema kuwa itasaidia kupunguza changamoto ya nyumba za kulala wagewni zenye hadhi ambazo zinahitajika hivi sasa kwa wingi jijini Dodoma.

“Kupatikana kwa hoteli hii katika jiji la Dodoma itatusaidia kuondoa usumbufu uliokuwepo hapo awali hasa wakati wa mikutano mikubwa ambayo wageni walikuwa wanapata shida kupata sehemu ya za kulala zenye hadhi ”amesema Prof. Mkenda

Aidha,Prof.Mkenda amesema kuwa wawekezaji wote ambao wanataka kuja kuwezakatika jiji la Dodoma milango ipo wazi kwani serikali itasaidia kufanikisha uwekezaji wao ili kusaidia kutoa ajira kwa makundi mbalimbali.

Pia amesema kuwa kwa sasa serikali imeweka mazingira wezeshi kwa mtu yeyote ambaye atahitaji kuja kuweza katika sekta mbalimbali.

Kwa upande wake Mbunge wa Dodoma, Antony Mavunde amesema kuwa jiji la Dodoma limejipanga kuhudumia wawekezaji ambao wataonyesha nia ya kuwekeza katika sekta mbalimbali.

Mhe.Mavunde, amesema kuwa hivi sasa kupitia baraza la madiwani wa Halamashauri ya jiji la Dodoma, wameweka mikakati ya kuhudumia wawekeza kwa muda mfupi na kuwapatia maeneo ya uwekezaji bila urasimu.

“Moja ya faida ya uwekezaji kama huu hapa jijini Dodoma ni kubadili muonekanao wa jiji letu lakini pia uwepo wa hoteli kubwa kama hivi kunasaidia kuondoa uhaba wa nyumba za kulala wageni hasa wakati ule tunapokuwa na mikutano mikubwa.

Naye Mkurugenzi wa Hoteli hiyo, Fladimiry Mallya,amesema kuwa anategemea kupata wageni wengi kutokana na huduma bora wanazotoa katika Hoteli hiyo ya kisasa katika Jiji la Dodoma.

Hata hivyo, ametoa wito kwa serikali kuwashika mkono wawekeza katika kuwasaidia kukabilina na kero mbalimbali ambazo wamekuwa wakikumbana nazo.

No comments: