Mratibu wa habari, elimu, mawasiliano na mabadiliko ya tabia Programu Shirikishi Ukimwi, Homa ya Ini, Kifua Kuu na Ukoma Zanzibar Ahmed Hani Mohamed akitoa muongozo wa mjadala kwa wanafunzi wa Skuli ya Afya Mbweni katika kongamano la maadhimisho ya siku ya Kifua Kikuu Duniani.
Msaidizi Meneja Programu Shirikishi Ukimwi, Homa ya Ini, Kifua Kuu na Ukoma (ZIHHTLP) Issa Abeid Mussa akifungua Kongamano kwa wanafunzi wa Skuli ya Afya Mbweni lenye lengo la kuibua wagonjwa zaidi wa Kifua Kikuu.
Baadhi ya wanafunzi wa Skuli ya Afya Mbweni wakifuatilia mada katika kongamano la siku ya kifua Kikuu Duniani lililofanyika Skuli ya Afya Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Dkt. Julios Obed akiwasilisha mada ya hali ya TB Zanzibar katika kongamano hilo.
Mwanafunzi Mwajuma Kheri anaesomea Uuguzi na Ukunga mwaka wa pili na mwenzake Onesmo Kaberwa anaesomea Udaktari wakichangia mada katika kongamano hilo lililofanyika Skuli ya Afya Mbweni.
Mratibu wa Mkoa kutoka Shirika la AMREF Dkt. Rahma Omar akitoa mchango juu ya nafasi ya wanafunzi wa kada ya afya kwenye kuongeza ugunduzi wa TB katika jamii.
Picha na Makame Mshenga.
Na Rahma KhamiS Maelezo
Jumla ya wagonjwa 1074 wa maradhi ya Kifua Kikuu (TB) wameripotiwa mwaka jana katika jamii baada ya uchunguzi uliofanywa na Programu shirikishi ukimwi, homa ya ini, kifua Kuu na ukoma Zanzibar.
Hayo yameelezwa na Mkufunzi Dkt Julius Obed katika Ukumbi wa Chuo cha Afya Mbweni wakati akitoa mafunzo katika Kongamano la Siku ya TB duniani lilowashirikisha wanafunzi wa kada mbalimbali katika Skuli ya Afya Mbweni.
Amesema idadi hiyo imeongezeka kutokana na baadhi ya wagonjwa wa zamani kujirejea tena maradhi hayo na kuifanya idadi hiyo kuwa kubwa na kupelekea wasiwasi katika jamiii.
Amesema kuwa Zanzibar mwaka 2012-2013 idadi ya wagonjwa 989 hadi kufikia mwaka 2020 wameongezeka sawa na asilimia 92 ambao ni wagonjwa hao ni wapya.
Aidha amefahamisha kuwa idadi kubwa ya wagonjwa wa maradhi hayo inatoka mjini na kwa upande wa Pemba inaongoza katika Wilaya ya Chakechake hivyo ipo haja kwa wahusika kuwafikia zaidi watu wa vijijini ili kupata idadi ya wagonjwa waliyoko huko.
Akifungua kongamano hilo Kaimu Meneja wa kitengo Shirikishi ambae pia ni Mwenyekiti wa Kongamano hilo Issa Abeid Mussa amesema kuwa lengo la kuadhimisha siku ya Tb Duniani ni kukumbuka ugunduzi wa bektiria mwaka 1982 anaesababisha maradhi hayo na pamoja na kuwapa taaluma wanafunzi ili kuibua wagonjwa.
Amesema siku hiyo hiyo ili kuielewesha jamii kutambaua uwepo wa maradhi ya TB na namna ya kujikinga kutokana na jamii kubwa kukosa uwelewa wa maradhi hayo.
Maadhimisho hayo huadhimishwa kila ifikapo mach 24 ambapo kwa mwaka huu wamefanya Machi 10 kutokana na kifo cha cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kaimu Issa amefahamisha kuwa katika mafunzo yao pia wanashughulikia maradhi ya mripulko ili kupambana nayo hivyo jitihada zaidi zinahitajika ili kuondosha kabisa maradhi ya TB ifikapo mwaka 2030.
Nae Mwakilishi kutoka WHO Dkt VendelinSimon amesema kuwa vita vya maradhi ya kifua kikuu ni lazima kila mtu kichukua juhudi ya kupambana nayo kuanzia familia na jamii kwa ujumla.
Aidha amezitaka Taasisi husika kushirikiana kwa pamoja na kuunda timu shirikishi na kutoa kazi ya kwa kufuatilia kazi katika maeneo ya vijini ili kuweza kutambua jinsi gani TB inapatikana na namna gani ya kujikinga na maradhi hayo.
Nao washiriki katika kongamano hilo wameiomba Wizara ya Afya kupitia kitengo shirikishi cha maradhi ya Ini,Ukoma Ukimwi na TB kufuatilia wagonjwa wa maradhi hayo majumbani ili kupambana na kudhibiti maradhi hayo yasienee katika jamii.
Katika kongamano hilo mada mbili zimejadiliwa, jinsi gani tutatambua wagonjwa Zanzibar na vipi Tasisi za elimu ya vyuo vikuu vitatokomeza TB ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni MUDA UNAPITA TUONGEZE MAPAMBANO DHIDI YA KIFUA KIKUU.
No comments:
Post a Comment