ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, June 2, 2021

BASI LA CLASSIC LAPATA AJALI BUYUBI - SHINYANGA


Watu watatu wanahofiwa kufariki dunia huku wengine wengine zaidi ya 30 wakijeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya Clasic kupata ajali eneo la Buyubi kata ya Didia barabara ya Kahama - Tinde Halmashauri ya Shinyanga mkoani Shinyanga.

Ajali hiyo imetokea usiku wa leo majira ya 10 alfajiri ambapo basi hilo lilikuwa likitokea Jijini Kampala nchini Uganda kuelekea Jijini Dar es salaam.

Wakizungumzia tukio hilo baadhi ya majeruhi wamesema kuwa ajali hiyo imetokea baada ya dereva kushindwa kuimudu kona ya Didia.

Mkuu wa jeshi la Polisi wilayani Shinyanga John Kafumu amefika eneo la tukio na kubainisha kuwa taarifa zaidi zitatolewa na kamanda polisi mkoani Shinyanga ACP Debora Magiligimba.

No comments: