Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa wilaya wa Mkalama Mhandisi Jackson Masaka funguo ya gari la kubebea wagonjwa katika Zahanati ya Wilaya ya Mkalama.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge (kulia) akisikiliza maelezo wakati akikagua jengo la wodi ya wazazi katika Zahanati ya Wilaya ya Mkalama.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM) Wilaya ya Mkalama Lameck Itungi akichangia jambo
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mkalama James Mkwega akiomba jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge
Na Edina Alex, Singida
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge amewataka watumishi wa umma kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuongeza ukusanyani wa mapato ya ndani.
Hayo yamejiri wakati alipokutana na kuongea na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Makalama kwenye ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo.
"Kama hukufanya vizuri wakati wa mtangulizi wangu sasa anza na Mahenge kwa kufanya kazi kwa bidii tusikate tamaa", alisema Mahenge.
Alisisitiza kuwa suala la ukusanyaji wa mapato ya ndani sio la mzaha na linamhusu kila mtu katika Mkoa wa Singida.
Aidha aliwataka watumishi na Chama Cha Mapinduzi ( CCM) kuvunja makundi yao na kuleta mabadiliko na kuendana na kasi ya Rais wa awamu ya sita Mhe. Samia Hassan Suluhu.
Akitoa taarifa ya maendeleo ya Wilaya, Mkuu wa wilaya wa Mkalama Mhandisi Jackson Masaka alisema Wakazi wa Mkalama wanakabiliwa na changamoto ya pembejeo ambayo iko juu hasa katika mbegu bora ya alizeti chotara ya Hysun 33 ambayo huuzwa kwa sh. 35,000 kwa kilo moja.
Aidha Masaka alisema Wilaya ya Mkalama ina changamoto ya maafisa ugani ,Magari na pikipiki na wakulima kutotumia vizuri mvua kidogo inayonyesha katika Wilaya hiyo.
No comments:
Post a Comment