Mkurugenzi
katika Wizara ya Afrika Mashariki na Maendeleo ya Kikanda ya Kenya na
Mwenyekiti wa Mkutano wa Ngazi ya Wataalam, Bi. Alice Yalla akizungumza
wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo uliofanyika jijini Arusha ikiwa ni
maandalizi ya Mkutano wa 31 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta
linaloshughulikia masuala ya Afrika Masahriki na Mipango katika Jumuiya
ya Afrika Mashariki unaotarajiwa kufanyika tarehe 11 Juni 2021.
Mkurugenzi
wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi akiongoza ujumbe
wa Tanzania kwenye mkutano wa majadiliano kwa ngazi ya wataalam
uliofanyika jijini Arusha tarehe 7 Juni 2021 kwa ajili ya kuandaa
Mkutano wa 31 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta linaloshughulikia masuala
ya Afrika Masahriki na Mipango katika Jumuiya ya Afrika Mashariki
unaotarajiwa kufanyika Arusha tarehe 11 Juni 2021. Mkutano kwa ngazi ya
wataalam unafanyika kuanzia tarehe 7 hadi 9 Juni 2021 na utafuatiwa na
Mkutano wa Makatibu Wakuu tarehe 10 Juni 2021. Kulia ni Mkurugenzi wa
Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji katika Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Benard Haule.
Naibu
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia Sekta ya
Uzalishaji na Jamii, Mhe. Christophe Bazivamo akifungua rasmi Mkutano wa
Ngazi ya Wataalam uliofanyika jijini Arusha kwa ajili ya kuandaa
Mkutano wa 31 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta linaloshughulikia masuala
ya Afrika Masahriki na Mipango katika Jumuiya ya Afrika Mashariki
unaotarajiwa kufanyika tarehe 11 Juni 2021
Ujumbe wa Kenya ukiwa kwenye mkutano wa ngazi ya wataalam
Sehemu ya ujumbe wa Tanzania ukishiriki Mkutano wa ngazi ya wataalam
Mkurugenzi
wa Idara ya Sera na Mipango katika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bibi Agnela Nyoni akifuatilia ufunguzi
wa mkutano wa wataalam uliofanyika Arusha kwa ajili ya kuandaa Mkutano
wa 31 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta linaloshughulikia masuala ya
Afrika Masahriki na Mipango katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)
unaotarajiwa kufanyika tarehe 11 Juni 2021.
Ujumbe wa Uganda ukiwa kwenye mkutano wa ngazi ya wataalam
Balozi
Mteule na Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bibi Caroline Chipeta
akifuatilia mkutano wa ngazi ya wataalam uliofanyika Arusha ikiwa ni
maandalizi ya Mkutano wa 31 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta
linaloshughulikia masuala ya Afrika Masahriki na Mipango katika Jumuiya
ya Afrika Mashariki unaotarajiwa kufanyika tarehe 11 Juni 2021.
Ujumbe kutoka Taasisi mbalimbali za Jumuiya ya Afrika Mashariki nao ukishiriki mkutano wa ngazi ya wataalam
Mkutano ukiendelea
Mjumbe kutoka Rwanda akiwa kwenye mkutano wa wataalam
Mjumbe wa Burundi naye akifuatilia mkutano
Sehemu ya ujumbe wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ukishiriki mkutano wa wataalam
Mkutano ukiendelea
Mjumbe kutoka Tanzania akishiriki mkutano wa ngazi ya wataalam
Mkutano ukiendelea
Mkutano wa 31 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (SCMEACP) unafanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 7 hadi 11 Juni 2021.
Mkutano huo ambao umeanza kwa Ngazi ya Wataalam leo tarehe 7 hadi 9 Juni 2021 utafuatiwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu utakaofanyika tarehe 10 Juni 2021 na kuhitimishwa na Mkutano wa Mawaziri utakaofanyika tarehe 11 Juni 2021.
Akifungua Mkutano wa Ngazi ya Wataalam, Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughilikia Sekta za Uzalishaji na Jamii, Mhe. Christophe Bazivamo amezipongeza Nchi Wanachama kwa kufufua viwanda vidogo na kutumia bidhaa za ndani hususan katika kipindi hiki cha janga la ugonjwa wa Corona ambalo limeathiri kwa kiasi kikubwa shughuli za uzalishaji na ufanyaji biashara katika nchi nyingi duniani zikiwemo zile za EAC.
Ameongeza kusema kuwa, ugonjwa wa Corona umetoa funzo kubwa kwa Nchi Wanachama wa EAC kwamba zinaweza kufanya biashara miongoni mwao na kujitosheleza kwa mahitaji mbalimbali ya msingi kwa maendeleo ya wananchi wa nchi hizo ikiwa ni utekelezaji wa Itifaki mojawapo muhimu ya Jumuiya ya Soko la Pamoja.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Mkutano huo wa Ngazi ya Wataalam, Bi. Alice Yalla kutoka Jamhuri ya Kenya amesisitiza wajumbe kujadili kwa umakini agenda mbalimbali zilizopo mbele yao na kutoa mapendekezo yenye tija, ikizingatiwa kuwa Sekta ya Mipango ni moja ya Sekta muhimu katika Jumuiya ambayo pamoja na mambo mengine pia hushughulika na tathmini ya mipango na masuala yote yanayotekelezwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mkutano wa Wataalam pia utapitia agenda mbalimbali muhimu ambazo zitawasilishwa kwenye Mkutano ngazi ya Makatibu Wakuu utakaofanyika tarehe 9 na 10 Juni 2021 kwa majadiliano na hatimaye agenda hizo zitawasilishwa kwenye Mkutano ngazi ya Mawaziri unaotarajiwa kufanyika jijini hapa tarehe 11 Juni 2021.
Miongoni mwa agenda hizo ni pamoja na Taarifa ya Utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa kwenye vikao vilivyopita; Taarifa kuhusu hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa Itifaki ya Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki; Kupitia maelekezo ya Baraza la Mawaziri kuhusu Rasimu ya Maboresho ya Utaratibu wa Mafao katika Jumuiya ya Afrika Mashariki; Taarifa kuhusu ombi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo la kujiunga na EAC; Taarifa kuhusu hatua iliyofikiwa ya utatu wa Jumuiya za EAC-COMESA-SADC katika Eneo Huru la Biashara Barani Afrika; Taarifa ya Uchangiaji wa Bajeti ya EAC kutoka Nchi Wanachama; na Taarifa ya majadiliano kuhusu Eneo Huru la Biashara Barani Afrika.
Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa Ngazi ya Wataalam unaongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi. Kadhalika Mkutano huo umehudhuriwa na Wajumbe kutoka nchi zote wanachama ambazo ni Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda na Sudan Kusini
No comments:
Post a Comment